Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 2,536
- 7,194
Jeshi la Polisi mkoani Morogoro limewakamata jumla ya watu 21 kwa tuhuma za kujihusisha na wizi na utapeli wa kimtandao unaojulikana kwa jina la “Halo Halo”, kufuatia operesheni maalum iliyofanyika kati ya Julai 2 hadi 11, 2025.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Alex Mkama, amesema watuhumiwa hao walikamatwa katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo, yakiwemo Ifakara (Kilombero), Msowelo na Rudewa (Kilosa), pamoja na Turiani (Mvomeru).
“Kati yao, 13 walikamatwa Ifakara, watano walinaswa Msowelo na Rudewa, huku watatu wakikamatwa Turiani,” alisema Kamanda Mkama katika taarifa yake ya Julai 14, 2025.
Amesema mtandao huo wa kihalifu umekuwa ukitumia mbinu mbalimbali, zikiwemo kusajili laini nyingi za simu kwa majina ya watu wengine kupitia mawakala wasio rasmi, kujifanya maofisa wa makampuni ya simu, waganga wa kienyeji, na hata wafanyabiashara wa mbolea na vyakula vya mifugo.
Aidha, Kamanda Mkama amewataka wananchi kujiepusha na tamaa ya utajiri wa haraka kwa njia zisizo halali na badala yake wafanye kazi zinazotoa mchango chanya kwa jamii na taifa kwa ujumla.