Hawa Members Maarufu kwa Fix/Kamba/Uongo, Ubishi na Kuwa wa Kwanza ku Comment

Hawa Members Maarufu kwa Fix/Kamba/Uongo, Ubishi na Kuwa wa Kwanza ku Comment

GuDume

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2015
Posts
6,651
Reaction score
14,337
Wadau kuna members humu ndani wana fix sana.... sijapata kuona.. yaani wanakufunga kamba mpaka mtu unajishtukia kabisa. huwa sometime utawashtukia namna wanavyojichanganya. kuna jamaa kaweka post yake sehemu .... aka changia anasema hawezi sahaau siku alipovamiwa na majambazi yeye akauawa akabaki mama na dada yake. anasema majambazi walimpiga risasi tatu kifuani akafa pale pale.

baadaye akakukumbuka kuwa yeye ndo alikuwa anatusimulia hiyo story akadelete haraka sana post. ila tulicheka sana. kuna jamaa humu wana IDs zaidi ya 5 yaani akitoa story ana log off kwa hii moja anaingia na nyingine kujisupport kuwa X umeongea kitu cha maana sana. we jamaa nakukubali. kumbe ni yeye mwenyewe. akakosea akaji quote kwa id ile ile akidhani amechange kaandika "mkuu nimeisoma thread yako ,duh nimekuelewa sana. mi kila ukianzisha thread nakuja kukusoma una madini mengi sana. hili jambo unalozungumzia ni kweli kabisa" hakujua kuwa ametumia ID ile ile aliyotumia kupost thread.

huwa nacheka sana.... kuna watu wana fix sana humu ndani lakini ndo raha ya JF siku zinaenda. halafu kuna jamaa wao wanakandia tu kila kitu hawa nao wapo. yaani wao kila kitu wanabisha na wanabisha mpaka kufa. huwa wanapokezana ubishi. mmoja anapo log off anamwambia mwenzie aendelee kubishana.

kuna jamaa mmoja nampenda yeye mara zote ni wa kwanza ku comment. huyu jamaa duh yupo faster sana. namkubali yaani hata hapa si ajabu akawa wa kwanza ku comment nasikia huwa akiona mwenzie amemzidi speed anamfuata inbox kumlalamikia kuwa hiyo nafasi ya kwanza ya comment ni yake.

halafu kuna kundi la watu wenye matusi... hawa ukiwashinda kwa hoja wanakujia inbox wanakutukana siku nzima yaani wao ni matusi tu ...kila ukiangalia meseji unakuta matusi.anaenda kuulizia matusi mapya huko anakuja tena anakutukana.. kuna dada anaitwa helloo huyu atakuwa na phd ana matusi huyu mwanamke acha kabisa.usije mchokoza umkamshinda kwa hoja.ukimshinda kwa hoja anakwambia sasa tushindane na matusi..anajua huko ata kutoa knock out tu. atakushinda. na anakushinda kweli.
 
Ukweli ni mzuri ila sio kila mahali...hapo ndo mwanzo wa ubaya

Sent from my GT-N7000 using JamiiForums mobile app
 
Jf ina mambo
Pitia huo uzi uone maajabu ya humu

HR 666 hujambo?
9560f4b579f6cb65c85290545077e83d.jpg
 
Mi nimewapenda hao wanaobisha hadi kufa, halafu kesho wanafufuka tena kuja kubisha....nafwaaaaaaa, mbavu zangu mie!
 
Back
Top Bottom