HORSE POWER
JF-Expert Member
- Feb 22, 2015
- 2,238
- 1,577
La hasha, hao si kioo jamii bali ni kivuli cha jamiiHabari wanajf!
Nina hoja fupi ningependa tujadili kidogo.Ni hili suala la wasanii wetu wa kiume;aidha wa muziki au filamu kuvaa hereni.Suala hili limeshika kasi na wale wanaoitwa chipukizi wanaiga bila ya kuhoji.
Sasa kwa maadili ya Kiafrika, wasanii wa namna hii wana sifa ya kuitwa kioo cha jamii? Wanapeleka ujumbe gani kwa watoto wetu?
Hapo sijazungumzia mivaaji ya wasanii wa kike.
Nawasilisha.