Hawa ndio mastar wa 5 wa bongo ambao wametoka familia za kishua

Hawa ndio mastar wa 5 wa bongo ambao wametoka familia za kishua

quote_icon.png
By lusungo
Huyo si mtoto Wa Tsere aliyekua mkurugenzi Wa AICC?

Ndio huyu amekulia kwamrefu jirani na cet garden bar halafu tsere hakua na makuu sasa stunna anakuja n ngonjera zake kua wa kishua

Hivi baba anaweza kuwa Mkurugenzi AICC halafu familia yake isiwe bora. maana kutokana na tafsiri ya mtoa mada... namnukuhu hapo chini

Hakuna mtu asiyejua maana ya watoto wa kishua basi kama yupo basi maana halisi ya neno hili ni wale watoto waliozaliwa kwenye familia zinazojiweza au unaweza kuita familia Bora.
 
Pale wengi wanakuaga alosto tu coz hela zenyewe za msimu....

Ila nawashangaa wabongo ushua wanautafsiri vipi MTU anaishi kikawaida tu wanabandika mabango...

Nasie wazee wetu walioanzia kwenye umeneja NMC hadi ukatibu mkuu Wa wizara tusemeje??

Maana bado najiona maskini tu...

nakupm wa kishua
 
historia haipigiwi makofi tunataka kuona nani anafanya nini for now....kimsingi tunakotoka is imaterial the point is now.
 
Hata mie wakishua, mzee Dg idaran fulani enzi za mwinyi, baloz usa, waziri kipindi cha ben, nimezaliwa usa, maisha bado nayaona magumu tu, ushua gan unazungumzia mtoa uzi😆😆
 
Sasa hivi ni mzee wa kishua amekuwa mwenyeji sana hapa duniani.
 
1526493_721531134526283_111801404_n.jpg



Hakuna mtu asiyejua maana ya watoto wa kishua basi kama yupo basi maana halisi ya neno hili ni wale watoto waliozaliwa kwenye familia zinazojiweza au unaweza kuita familia Bora. Mara nyingi wasanii wengi huwa wanatokea maisha duni na kupigana na maisha hadi kufikia walipo sasa. Kipindi Diamond akiacha shule kwa kukosa pesa ya kumsomesha nana elimu yake kuishia A’level , Hawa wengine walikua wapo shule wakisoma na kuishi vizuri. Vibe Tanzania inawaorodhesha baadhi ya watoto wakishua ambao kwasasa ni celebrities…


Vanessa Mdee

Vanessa Hau Mdee au unaweza kumuita Vee au Vee Money alizaliwa mjini Arusha mwaka 1988. Vanessa mdee alikuzwa na baba yake Sammy Mdee (kwasasa ni marehemu )ambaye alikua ni mtu mzito kwenye nchi hii na mama yake sophia. Akiwa na umri mdogo Vanessa aliweza kusafiri nchi mbalimbali duniani. Vanessa Mdee alikulia miji ya New York , Paris , Nairobi na Arusha.


Nisher
Nisher ni mtoto wa Mtumishi wa Mungu Mh Nabii GeorDavie anayeongoza huduma ya Ngurumo ya Upako yenye makao yake jijini Arusha. Nisher amekulia katika maisha mazuri na hadi ni wakishua bado. Baba yake aliweza kumsaidia Nisher kufungua studio yenye thamani kama ya milioni 15 ili mtoto wake aendeleze kipaji alichonacho.


nisher-5.jpg


Jokate Mwengelo
Huyu unaweza kumuita mtoto wa Oysterbay kwani ndio alipokulia huku baba yake akifanya kazi serikalini. Kumbuka Jokate alizaliwa washington DC nchini Marekani ambapo wazazi wake walikua wakifanya kazi huko. Alipomaliza high school katika shule ya Loyola ndipo alipogombania Miss Tanzania mwaka 2006 na kushika nafasi ya 2.

kidoti.PNG


Lucci

Jina lake halisi anaitwa Luciano Tsere au unaweza kumuita Lucci ambaye ni producer maarufu nchini. lucci amezaliwa tarehe 30 September mwaka 1985 Lusaka Zambia, akiwa ni mzaliwa wa nne, wa mwisho kuzaliwa na akiwa mtoto wa kiume pekee kwenye familia yao. Lucci naye kama jokate amekulia Obey kwenye familia bora ambapo kwasasa mzee wake ni balozi wa Tanzania.

lucciphoto.jpg


Wema Sepetu
Wema Sepetu ni msichana anayetoka kwenye Familia ya kibalozi akiwa ni mtoto wa mwisho katika familia ya wasichana wanne wa Balozi Isaack Sepetu Ibrahimu (marehemu).Wema sepetu alizaliwa mnamo mwaka 1988 katika hospitali ya ST. Andrew’s jijini Dar es Salaam na ni mtoto wa mwisho kuzaliwa huku akisoma elimu yake ya primary na sekondari katika shule ya ACADEMIC INTERNATIONAL iliyopo jijini Dar es Salaam kabla ya kwenda Nchini Malaysia kusomea mambo ya biashara za kimataifa katka chuo cha Limkokwing University.

Wema mshaona sana picha zake ndio maana hapa sijaiweka


wewe mwenyewe star ( wa jamii forum) na unatoka familia bora mara nyingi ukija bongo hupiti Airport ya Dar wewe unaenda direct Nairobi zen unachukua basi unakuja bongo. hahahahahaua hivi mbona hukushiriki big brother?
 
hiro rinisher kama vire rinavuta bange hebu riangarie sura yake , arafu hii mitoto ya wachungaji inakuwa na tabia mbofu mbofu richeki hiri rimeweka hereni kuna rile ringine rinajiita rinah kazi kuva nguo fupi fupi
 
"Kuna tofauti gani kati ya temeke na mbezi? ama ukiishi mbezi utakapokufa hauozi?/haipendezi eti kutomjali mwenzako kwasababu ya mavazi,au sababu ya makazi!"
Darubini by Afande selle
 
Hivi mbona wamemsahau King Kiba 🏃🏃
 
Back
Top Bottom