Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Feisal 'Fei Toto' Salum - Azam FC
Katika dirisha la usajili la kiangazi Julai 2024, Fei Toto alihusishwa na klabu kubwa Afrika kama Mamelodi Sundowns na Kaizer Chiefs kutoka Afrika Kusini, Wydad Athletic Club ya Morocco, pamoja na Simba SC. Hata hivyo, dau lake la TSh bilioni 5.1 (kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Azam FC, Hashim Ibwe) lilikwamisha uhamisho wake. Fei Toto ana mkataba na Azam FC hadi mwaka 2026.
Pia, Soma:
• Fei Toto apokea Ofa ya Tsh Milioni 600 kutoka Simba SC kwa Mkataba wa miaka Mitatu
Kibu Denis - Simba SC
Thamani yake iliwahi kuwekwa wazi na Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally, kuwa ni TSh bilioni 2.5+, baada ya sakata lake la kutorokea Norway 🇳🇴 muda mfupi baada ya kuongeza mkataba wa miaka miwili Simba SC mpaka Juni 2026 kwa TSh 300 milioni.
Clement Mzize - Yanga SC
Mshambuliaji huyu alitikisa vichwa vya habari Afrika mwishoni mwa wiki iliyopita (Jan. 4) kwa kuisaidia Yanga kufufua matumaini ya kutinga Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Aliifungia magoli mawili kwenye ushindi wa 3-1 dhidi ya TP Mazembe. Clement alitajwa kuwa kwenye ofa kutoka Wydad Athletic Club ya Morocco kwa dau la zaidi ya TSh bilioni 2.
Soma:
- Wydad waongeza 1.4Tsh billion Kwa mzize
- Yanga imekataa ofa ya pili ya klabu ya Wydad ya Tsh Bilioni 1.7