Hawa ndio wanamichezo wangu Bora 22 ndani ya Tanzania kwa Karne ya 21

Hawa ndio wanamichezo wangu Bora 22 ndani ya Tanzania kwa Karne ya 21

mugah di matheo

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2018
Posts
6,307
Reaction score
12,410
Karne ya 21 tumeshuhudia mengi Sana kwenye michezo,ya kutia aibu mfano kukosekana kwa disc lenye wimbo wa taifa ndani ya uwanja wataifa Hadi yale ya kubadilisha muda wa mchezo bila timu shiriki kupewa muda.
Pia Kuna mengi mazuri ya kujivunia ndani ya miaka hii 22 ya Karne ya 21.

Wafuatao ni wanamichezo Bora wa Karne ya 21 wenye uraia wa Tanzania.

22.Makore na Agwanda(kotinyo)
Wanapambania Sana basketball ya nchi hii

21.Shafii Dauda
Anapambana kuibua na kuendeleza michezo kupitia Ndondo cup na shadaka

20.Thomas Ulimwengu
Mafanikio ni kubeba Cafcl na Cafcc akiwa Mazembe.
Kushiriki Afcon akiwa na stars.
Miongoni mwa wachezaji wenye magoli mengi timu ya taifa

19.Jay msangi
Promota mwenye kashfa nyingi Sana za upigaji Ila ndio kawafungua macho mabondia wetu.

18.Charles Mkwasa
Miongoni mwa makocha wazawa wanaofanya vizuri ligi kuu
Kuwa kocha wa national team
Kuwa kocha wa zesco

17.Kelvin John
Kinda wa kitanzania hapo Krc Genk

16.Opah Clement
Mchezaji toka twiga stars

15.George Kavila
Anarekodi ya kuchezea timu moja kwa misimu mingi zaidi kwenye ligi ,miaka 21 kwa kagera sugar.

14.Masau Bwire na Thobias Kifaru
Wasemaji Bora wa muda wote na wanaojua kubrand timu zao.

13.Faulina Abdi
Licha ya kutokuwa na medali lakini ni mwanariadha Bora wa kike nchi hii

12.Aishi Manula
Golikipa bora Sana ameendelea kuonekana.
Ndio Golikipa wa kwanza kucheza Quarter final ya ccl na Ccc ndani ya Tanzania na kucheza Afcon pia(I mean vyote vitatu kwa pamoja)

11.Fredy Mbuna
Kudumu kariakoo kwa misimu 15 kwahitaji Moyo Sana

10.Abdi kasimu ''Balack wa unguja"
Ni mtanzania wa kwanza kufunga goli uwanja wataifa saivi kwa mkapa.
Mtu wa kwanza kufunga goli ni raia wa Mozambique

9.Juma kaseja
Anarekodi za cleensheet nyingi ligi kuu
Ana kombe la challenge cecafa na taifa stars
Robo fainali ya ccl 2003 akiwa na Simba.
Ubingwa bila kufungwa msimu mzima

8.John Bocco
Mfungaji bora wa muda wote wa ligi kuu

7.Mrisho Ngassa
Mfungaji bora wa muda wote wa Taifa stars


6.Leodigar Tenga
Rais wa tff aliendesha Tff bila upendeleo.
Mjumbe wa Caf ,rais wa zamani wa cecafa ya mwisho kuendesha mashindano

5.Mo dewji,Bakhresa na Zachary Hanspope
Mo na Bakhresa kwa uwekezaji

Hansi kwa umaridadi wake katika usajili.

4.Alphonce Simbu
Mwanariadha anayepambana Sana na Bora kwa muda wake

3.Hasheem Thabeet
Kucheza NBA

2.Samata
Sina Cha kumuelezea

1.Mwakinyo
Mikanda kede kede kwenye Boxing

Asanteni Sana, Unaonaje wewe na maoni yako ni yapi?
 
Eti Nini...!? Mwakinyo!? Rudia tena kuandika uzi wako
 
Hii ni hadithi Ya 'Kumbi na Kumbinga'....

Itafute uisome...

Mmoja alisema tembo anafanana na Ungo...huyo alishika Sikio la Tembo

Mwingine akasema tembo anafanana na Ukuta..huyo alishika ubavu wa tembo.

Hata baba ake Haji hujamtaja aliitwa Computer wakati hata computer zenyewe zile zenye chogo zilikuwa bado kuingia nchini, we unakuja kututajia Shafi..?
 
Baraka mpenja na Mwalim Kashasha r.i.p watangazaji wa mechi.
Ahmedy Ally semaji la CAF 👈😂😅.

Injinia Hersi kiongozi bora wa club kwenye usajili.🏃🏃🏃.

G.S.M & Yusuf Bakhresa wawekezaji wanaotoa fedha bila mbwembwe na malalamiko mengi kama wahindi🙆.

Jonesia Rukyaa a.k.a mama Baleke kocha bora wa kike kwenye mechi za Simba na Yanga👍.
 
Back
Top Bottom