Hawa ndio wanaokwamisha Nchi; Makasuku na Wanafiki

Hawa ndio wanaokwamisha Nchi; Makasuku na Wanafiki

Chakaza

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2007
Posts
40,455
Reaction score
73,145
Je, mnadhani kama hawa makasuku na wanafiki ambao hata serikali ikipotoka na kukosea wana tumia nguvu kuunga mkono wasingekuwapo nchi hii ingekuwa imefika wapi kimaendeleo? Ni wazi kwa kujitambua na mijadala huru ingetokea basi taifa lingekuwa mbali sana.

JK alitaka Bagamoyo Port wakashangilia sana, JPM aka crash hilo wazo wakabinuka hadi sarakasi kumuunga mkono. JPM akazuia shughuli za kisiasa wakaandamana eti hapa kazi tuu na viongozi/wabunge mchongo wakakamaa shingo kuunga mkono lakini Samia kaleta maridhiano basi hao hao ndio bila aibu wako mbele kusema JPM alifungia nchi na sasa wanaweka mabango kuwa maridhiano ni kitu bora.

Limekuja la Bandari, angalia jinsi wanavyo wabeza wanaofanya mijadala ya hofu ya mkataba huo. Hawajibu hoja bali wanaleta vioja tuu. Sasa Waziri mkuu (PM) kama kiongozi wa serikali kaja na kauli kuwa mawazo mbadala na hofu ya wananchi yatachukuliwa na serikali na kufanyiwa kazi.

Sasa tusubiri MAKASUKU na WANAFIKI watasema nini tena! Bila hawa nchi hii ingefika mbali.

IMG-20230620-WA0025.jpg
 
Hii nchi % kubwa ni watu wasiojielewa, hawajui kuhoji wala kuchukua hatua na ndio iwe serikali iwe bunge au taasis yoyote wanaweza kuongea jambo la ajabu kabisa aibu coz wanajua majority ni kama hawapo timam zaidi ya kufuatilia pretty issues kama mipira na scandals za wasanii
 
Sasa Waziri mkuu (PM) kama kiongozi wa serikali kaja na kauli kuwa mawazo mbadala na hofu ya wananchi yatachukuliwa na serikali na kufanyiwa kazi.[emoji419][emoji375]

Sent using Jamii Forums mobile app
Kumbe ndio maana PM alikuwa kimya muda mrefu ili vuvuzela wabwabwaje kwanza aone upepo umekaaje na alipoona wapingaji wana hoja zao kajitokeza.

Hii ni aibu kwa Gerson Msigwa na timu yake ya machawa.
 
Huyu ndiyo rais 2025. Ameamua kusimama na wananchi bila kujali kibarua chake. Asante pm
 
JK alitaka Bagamoyo Port wakashangilia sana, JPM aka crash hilo wazo wakabinuka hadi sarakasi kumuunga mkono. JPM akazuia shughuli za kisiasa wakaandamana eti hapa kazi tuu na viongozi/wabunge mchongo wakakamaa shingo kuunga mkono lakini Samia kaleta maridhiano basi hao hao ndio bila aibu wako mbele kusema JPM alifungia nchi na sasa wanaweka mabango kuwa maridhiano ni kitu bora.
Tujifunze kupitia makosa 2025 tuwajue nani wa kuwanyoa kwa chupa, nani wa kuwanyoa kikavu kwa wembe na nani wa kuwanyoa kwa mkasi, hii nchi kuiongoza ni rahisi sana iwapo tu viongozi watakuwa wawazi, wakweli, wanasimamia katiba na sheria zetu, matatizo yote tunayopitia ni kwasababu ya njaa za watu wachache wanaotazama zaidi interest zao
 
Bahati mby sana nchi imejaa wajinga wengi ambao hao ndio wapiga kura wao wa kuwaweka madarakani
 
Back
Top Bottom