Hawa ndio wasanii watano Africa wenye kipato kikubwa

Hawa ndio wasanii watano Africa wenye kipato kikubwa

Mkuu isho_boy,

Nadhani unafahamu mimi ni WCB 'kindaki ndaki' lakini hiyo list huyo mwandishi amekosea sana.. Kimuziki ukiniuliza wasanii watatu wakali Afrika kwa mwaka 2016 nitakwambia Chibu ni mmoja wapo, lakini ukiniuliza wasanii 10 wenye hela Afrika.. Nakuhakikishia Diamond hayumo.. Nitatoa sababu

Hiyo list imefanya uchambuzi juu juu sana pasipo kuzingatia masuala muhimu.. Wamefanya makosa yafuatayo;

1. Kuna methodology zinazotumika kupata 'net woth' ya mtu na moja ya vitu vya msingi kabisa unavyotakiwa kuviepuka ni kutojumuisha 'primary residence' (nyumba anayoishi) katika mahesabu ya networth..
Hii ndio njia ndio inatumika na Forbes kukokotoa utajiri wa mtu! Hautakiwi kujumuisha vitu binafsi (nyumba anayoishi, gari anayotembelea na vitu kama hivyo)

Unachotakiwa kukokotoa ni 'vitega uchumi' na fedha zilizopo bank au shares kwenye makampuni..
Kwamfano hapo wanasema akothee ana utajiri wa biln 132.. Kiuhalisia makampuni ya Akothee huko Kenya yana valuation ya dola milioni 10 pekee lakini ukijumlisha na nyumba ya Switzerland aliyopewa mwanzoni mwa mwaka ndio labda unapata hiyo figure (nyumba inasemekana ina valuation ya dola milioni 50).

Sasa kwa standard za Forbes kwa mfano unatakiwa ukokotoe valuation ya makampuni yake pekee pasipo kujumlisha nyumba yake UNLESS nyumba ile haishi bali anaitumia kibiashara. (Kukodisha, kupangisha n.k)

Kosa hilo hilo wamelifanya kwa chibu kujumlisha ikulu yetu ya Madale na Jumba la Pretoria. Zile ni primary residence haziingii kwenye hesabu za net worth. Wanachotakiwa kufanya ni kufanyia valuation kampuni ya WCB kisha kukokotoa thamani ya shares za Chibu kwenye WCB ndio wajumlishe kwenye hesabu za net worth yake.
Tatizo la masupastaa wetu wengi Africa ni kutozifanyia valuation kampunj zao, ndio maana huwezi kukuta matajiri wakubwa wanaenda kuwekeza kwa kuingia ubia au kununua shares kwenye kampuni zao.. Tajiri anaye jielewa kabla hajawekeza mahali kwanza anataka kujua thamani ya hiyo kampuni..
Yani mfano umshtukize Simba sasa hivi umuulizs WCB market value take ni kiasi gani?? Hajui..

Kingine hiyo mikataba ya voda, sijui dstv, sijui Coca cola, nayo wamechukulia juu juu.. Wamejumlisha tuHawajaondoa kodi aliyolipa baada ya yeye kulipwa, hawajaondoa 'kipande' cha akina babu tale, sallam, fella, Zari.. Unaona kosa hilo??

Kwenye kiwango cha malipo ya shoo ndio wamebugi kabisa?? Eti diamond analipwa mln 25 kwa show akiwa ndani ya nchi?? Nani kakwambia?? Ameshavuka hicho kiwango.. Ni dhahiri huyo mwandishi amechukua habari za kwenye mablogu pasipo kutafiti!


2. Kwa Nigeria ndio wamevurunda kabisa! Mfani Don Jazz ana utajiri mkubwa kuliko Wizkid na Davido, kwanini hayuko kwenye list? Vipi kuhusu Banky W?? D'banj??

Tutofautishe kuwa maarufu au kuhit kwenye chart za muziki na utajiri. Ndio maana drake anahit zaidi ya Diddy lakini kwenye hela anasubiri miaka mia nane.
Hii ndio kama Don Jazz huyu jamaa amejijenga haswa kibiashara, Davido na Wizz bado sana kumfikia kwa fedha..

Alafu huyo mwandishi amewahi kumsikia mtu anaitwa Fally Ipupa??


Kama nilivyosema mimi ni WCB kindaki ndaki na lengo langu sio kuponda Chibu, ila tukiamsifia kwa vitu vya uongo tunamuharibu, atabweteka wakati vitu vyenywe vya uongo.. Tukimwambia ukweli kama hivi ndio ataendelea kupambana na sisi tulio karibu nae tunaongeza vitambi..


The Bold.

# WCB # Winners Cycle
Mkuu umekosea San kukoment kwenye hii mada ungekomenti mwishonimwishon uko kaka.....umewapa watu kitu cha kuongea
 
Unajua iyo show alilipwa hela sawa na aliyolipwa Vanessa mzee 2m ksh.....au ndo zen hampendi show off
Diamond akijitahidi kufanya kazi nzuri zaidi na juhudi huenda mwakani akachukua namba 1 kwa Africa nzima.
 
Nyie watu wa mikoani mna tabu mno ila sisi tulio mjini tunajionea wenyewe.Huwezi kumdanganya mtu wa mjini na akakubali kuwa Dimond ana Bilioni 4 kwenye account yake.

Dimond kila siku analia kutaka kumiliki Royce Rolls na hizo bei zake zilivyo kana angekuwa na kipato cha hivyo na alivyokuwa mpenda sifa angezinunua hata 2 kwa mpigo ili awarushe roho wabaya wake ila leo hii gari ya thamani anayomiliki ni BMW x6 tena tena used aliyopewa zawadi na uongozi wake.

we toka unamjua Dimond ushawahi kusikia hana Hisa japo kwenye kampuni ya Kutengeneza Ndala?!
Sasa utakubali mtu mwenye mabilioni asiwekeze hela yake kwenye makampuni ikazunguka yaani ikae tu bank kwani kimekuwa kichwa kile kila anapokwenda awe nacho?!

List yako ya kiboya na ya uongo mtupu wapi Casper vyovest hapo,Wapi Don Jazzy wapi D Banj wapi Mr.Flavour wapi A.k.A wapi Fally Ipupa wapi Koffi Olomide?!

Umekurupa siku nyingine ukidanganywa huko fikiria kwanza kabla ujataka kudanganya na wengine.

Yote yote asante kwa taarifa nenda Madale kachukue buku 7 yako.
 
Kweli pata pesa tujue tabia yako. Yan diamond anaingia mara 30 kwa pesa ya psquare. !!!!!!!!! Ila kwa mbwebwe anawazidi mara 100
Unawezaje kuwafahamisha PSquare na Diamond kwa kipato? PSquare wameanza 1999, Diamond kaanza 2009, sasa how possible wakawa na kipato sawa. Halafu mbwembwe za Diamond ndizo zinazompa pesa, angekuwa hana mbwembwe asingekuwa msanii ghali Tanzania na East Afrika.
 
mondi na masanja nani anamula ndefu kumshinda mwenzie
Kwa sie tulio mjini hapa tunaona kabisa kuwa Masanja ana pesa ndefu kuliko Dimond ila hawa majamaa wa mikoani wanaona kuwa Dimond ana pesa kuliko Masanja tusiwalaumu kwa sababu wenyewe wanaamini ukiwa maarufu zaidi basi lazima utakuwa na pesa zaidi.
 
mondi na masanja nani anamula ndefu kumshinda mwenzie
Kwa sie tulio mjini hapa tunaona kabisa kuwa Masanja ana pesa ndefu kuliko Dimond ila hawa majamaa wa mikoani wanaona kuwa Dimond ana pesa kuliko Masanja tusiwalaumu kwa sababu wenyewe wanaamini ukiwa maarufu zaidi basi lazima utakuwa na pesa zaidi.
 
Nyie watu wa mikoani mna tabu mno ila sisi tulio mjini tunajionea wenyewe.Huwezi kumdanganya mtu wa mjini na akakubali kuwa Dimond ana Bilioni 4 kwenye account yake.

Dimond kila siku analia kutaka kumiliki Royce Rolls na hizo bei zake zilivyo kana angekuwa na kipato cha hivyo na alivyokuwa mpenda sifa angezinunua hata 2 kwa mpigo ili awarushe roho wabaya wake ila leo hii gari ya thamani anayomiliki ni BMW x6 tena tena used aliyopewa zawadi na uongozi wake.

we toka unamjua Dimond ushawahi kusikia hana Hisa japo kwenye kampuni ya Kutengeneza Ndala?!
Sasa utakubali mtu mwenye mabilioni asiwekeze hela yake kwenye makampuni ikazunguka yaani ikae tu bank kwani kimekuwa kichwa kile kila anapokwenda awe nacho?!

List yako ya kiboya na ya uongo mtupu wapi Casper vyovest hapo,Wapi Don Jazzy wapi D Banj wapi Mr.Flavour wapi A.k.A wapi Fally Ipupa wapi Koffi Olomide?!

Umekurupa siku nyingine ukidanganywa huko fikiria kwanza kabla ujataka kudanganya na wengine.

Yote yote asante kwa taarifa nenda Madale kachukue buku 7 yako.
Povu linavokutoka sasa hahahhaaaa mm nacheka tu
 
itakuwa ni timu WCB hao wamezudisha mahaba kwa simba mbarara
Kwa sie tulio mjini hapa tunaona kabisa kuwa Masanja ana pesa ndefu kuliko Dimond ila hawa majamaa wa mikoani wanaona kuwa Dimond ana pesa kuliko Masanja tusiwalaumu kwa sababu wenyewe wanaamini ukiwa maarufu zaidi basi lazima utakuwa na pesa zaidi.
 
Kwa hiyo kiwango cha mwisho cha wasanii 5 bora wenye pesa afrika kinaanza na bil 9 za diamond then anafuata wizkid bil 24?...kutoka 24 had 9 sitaki kuamininkama hapo katikati hakuna namba nyingine ningependa kujua kuhusu fakky ipupa na d banji nataka nijue Leo kama diamond kawazid kioato ili nichekeeee...or niweke sawa hizi takwimu ni zako binafsi or umefetch somewhere?..Kofi olomide?..aaaah broooooooh
 
Leo hii diamond kamzidi d banj, Kofi, etc hapana lazima Luna ujanja ujanja kwenye hii list sio bure
 
List halisi na ya ukweli ni hii
1.YOUSSOU NDOUR-SENEGAL
2.P-SQUARE-NIGERIA
3.D BANJ-NIGERIA
4.KOFFI OLOMIDE-CONGO
5.SEIF KEITA-MALI
6.FALLY IPUPA-CONGO
7.2 FACE IDIBIA-NIGERIA
8.HUGH MASEKELA
9.BANK W-NIGERIA
10.JOSE CHAMELEON-UGANDA.
 
Mara nyingi tumezoea kuona list za wasanii wakubwa wakitajwa kuingiza pesa nyingi zaidi Afrika, wiki hii imetoka list iliyoandikwa naeDaily kupitia ripota Brian Okoth ambayo imewataja wasanii watano kutoka Afrika wanaotajwa kuingiza pesa nyingi zaidi mwaka 2016.

5. Diamond Platnumz (Tsh. Bilioni 9,665,923,190.55)

xdiamond1.jpg.pagespeed.ic.Kwk283qj2M.jpg
c.jpg
Mtanzania Diamond Platnumz huenda akawa msanii anayezungumzwa au kutajwa sana kwasasa barani Afrika kutokana na headlines anazotengeneza kila siku, mikataba yake na makampuni makubwa kwenye kazi zake pia inazidi kumuweka sehemu nzuri kifedha.

Hakuna shaka kwamba Diamond ni mmoja kati ya wasanii wanaoingiza pesa nyingi kupitia muziki wao kwasasa, na hili litaondoa utata kuhusu kiasi cha pesa alichotajwa kuwanacho staa huyu wa single ya Make Me Sing ambaye aliwahi kuzungumza na E!TV Jumapili ya, June 26 mwaka huu na ikaelezwa kuwa anamiliki pesa zinazozidi kiasi cha dola Milioni Nne za Marekani (Zaidi ya Bilioni 9 za Tanzania).

Kiasi hicho cha pesa hakijaja tu kama suprise kwa Diamond, ambaye anatajwa kuwa ndiye msanii anayelipwa pesa nyingi zaidi kwenye show au event yotote anayotakiwa kuhudhuria nchini Tanzania na pengine Afrika Mashariki kwasasa.

Pesa nyingi zinaelezwa kuingia kupitia shows alizofanya ndani ya Tanzania, East Africa na nje ya Afrika. Diamond Platnumz pia amekuwa balozi wa makampuni mengi makubwa ya biashara ikiwemo Vodacom, Cocacola, DSTV, Uber Taxi na Red Gold.

Ziko taarifa kuwa Diamond Platnumz huchaji si chini ya shilingi milioni 25 kwa show moja ya kawaida akiwa Tanzania, pia gharama hizo hufikia shilingi milioni 50 na kuendelea akiitwa na kampuni ya biashara na kama akiitwa nje ya Tanzania basi gharama zake huanzia shilingi milioni 200 na kuendelea.

Vyanzo vingine vya mapato ni pamoja na mauzo ya miito ya simu ambayo inaelezwa hakuna msanii yeyote Afrika Mashariki anayefikia mauzo yake kwenye ukanda wa maziwa makuu, pia anamiliki akaunti ya Youtube ambayo ipo kwenye list ya chaneli 10 zinazoangaliwa zaidi barani Afrika.

Hivi karibuni Diamond Platnumz ameingia kwenye biashara za kununua nyumba za zamani na kuzifanyia ukarabati ambapo huzipangisha, kitu kinachotajwa kumuingiza mkwanja mrefu zaidi jijini Dar es salaam, mbali na kumiliki record lebel yake ya Wasafi Classic Baby (WCB) ambayo kwa mujibu wake Diamond aliwahi kusema wamesaini deal ya zaidi shilingi Bilioni 2 na lebel ya Universal Music Group ya Marekani ili kusambaza kazi za wasanii walioko chini yake ambao ni Rich Mavoko, Harmonize na Rayvany.

4. Wizkid (Tsh. Bilioni 25,676,809,453.47)
image.aspx


Kwa mujibu wa Infoguide Nigeria, mpaka kufikia December 2015 mwimbaji star Wizkidalikuwa anakadiriwa kumiliki kiasi cha dola Milioni 11.5 ambazo mpaka mwisho wa mwaka 2016 inaelezwa kuwa amefikisha dola Milioni 12.

Wizkid amekuwa na mikataba inayomuingizia pesa nyingi na makampuni kutoka Nigeria ikiwemo label yake ya Star boy Recordsaliyoianzisha mwaka 2010. Pia mwaka 2014 Wizzy alisaini deal ya kuwa balozi wa kampuni ya simu ya MTN ambao walimlipa zaidi ya shilingi milioni 300 na kampuni ya MTN rival Globacom ikapanda mara mbili ili kumtumia Wizkid kama balozi wao.

Deal hiyo ya miaka miwili inatajwa kumuingiza Wizkid zaidi ya shilingi milioni 900 kutoka kampuni ya Globacom na mwaka 2015 wakati akifanya sherehe ya kutimiza miaka 25 Wizkid alisaini upya mkataba wake na kampuni ya vinywaji baridi ya Pepsi.

Ukijumlisha kiwango cha pesa anachoingiza kutoa kwenye shows anazofanya, mauzo ya nyimbo zake, tuzo, zawadi pamoja na mikataba yake, inamuweka star huyo kwenye list wasanii wanaoingiza pesa nyingi zaidi nchini Nigeria. Zipo taarifa kuwa ili kuweza kumualika Wizkid aje kufanya show ya kampuni itakubidi umlipe si chini ya shilingi milioni 60.

Kumbuka pia mwezi August, 2015, WizKid alitajwa kwenye jarida la Forbes kama miongoni mwa mastaa 14 wanaoitangaza Afrika.

3. Davido (Tsh. Bilioni 30,502,418,406.03)
maxresdefault.jpg
Kwa mujibu wa Nigerian Finder wameeleza kuwa Davido anamiliki utajiri unaofikia dola milioni 14 ambazo ni zaidi ya shilingi Bilioni 30 za Kitanzania.

Pamoja na kuzaliwa kwenye familia yenye uwezo mkubwa kifedha, hiyo haikumfanya Davido kurelax badala yake alitumia nafasi yake kama msanii kujenga jina lake na kufanya biashara inayomfanya kuingiza pesa nyingi kwenye akaunti zake.

Mwaka 2012, Davido alisaini deal na kampuni ya MTN TV kama balozi na akasaini deal nyingine na MTN Pulse kuwa muwakilishi wa kampuni hizo kwa kitita cha zaidi ya shilingi milioni 207 za Kitanzania, wakati huo huo mwaka 2014, Davido alilipwa zaidi ya shilingi milioni 341 kuwa balozi wa kampuni ya dawa za meno ya Close UP.

Pia Davido na kaka yake Adewale Adeleke wanamikili lebel ya muziki iitwayo HKN Music ambayo imekuwa ikiwaingiza pesa nyingi kupitia mauzo ya nyimbo za wasanii waliosaini lebel, mauzo ya albam pamoja mikataba ya matangazo.

2. Akothee (Tsh. Bilioni 132,683,540,000.00)
Screenshot-from-2016-08-31-145647.png


Akothee%E2%80%99s-home-in-Rakwaro-Migori-County.jpg
Huenda ikakushtua sana kutokana na jina la msanii huyu kutokua kubwa sana au kutofahamika sana kwa watu wengi, Mwimbaji Akothee kutoka Kenya anatajwa kuwa na utajiri unaofikia dola za Marekani milioni 61 ambazo ni zaidi ya shilingi za Tanzania Bilioni 132.

Mapema mwaka huu, mitandao ya habari za mastaa nchini Kenya iliripoti kuwa star huyo wa single ya Give It To Me alikuwa anamiliki zaidi ya shilingi za Tanzania Bilioni 8.

Akothee amekuwa akijishughulisha na biashara pamoja na kilimo huku chanzo kingine cha mapato kikitajwa kuwa ni fidia aliyolipwa kama talaka na mwanaume wa kizungu aliyeachana naye miaka kadhaa iliyopita.

1. P-Square (Tsh. Bilioni 277,752,822,639.34)
922.jpg


psquare.jpg


Wakiwa ni mastaa pekee kutoka Afrika kutajwa na jarida la Forbes mara mbili kwenye list ya wasanii wanaolipwa pesa nyingi zaidi Afrika, kundi la PSquare limeendelea kuweka rekodi ya kufanya shows za gharama kubwa kupita wasanii wote Afrika, huku wakipata mialiko kutoka kwa Marais wa nchi zaidi ya 5 na usisahau, mastaa hawa wanamiliki ndege binafsi.

Kwa mujibu wa jarida la watu maarufu la Forbes, mapacha hao Peter na Paul Okoye wanaounda kundia la P-Square wanamiliki utajiri wa zaidi ya dola za Marekani milioni 130 zinazotokana na mikataba ya kibiashara na makampuni mbambali, biashara za mafuta, mauzo ya muziki na shows wanazofanya.
Usirudie kupost utumbo bila koffi
 
Back
Top Bottom