Hawa ndio wasomaji makala wenye sauti ya mvuto Tanzania

Hawa ndio wasomaji makala wenye sauti ya mvuto Tanzania

Kama ningetaka kutaja 10 ningeongeza hawa
Shaban Kisu TBC
Alex Muridhi BBC
Ahmed Dahman DW

Huyo namba tatu alishafariki.

RIP Mohamed Dahman.


Taarifa za kifo cha mtangazaji mwenzetu Mohammed Dahman, aliyeaga dunia siku ya Ijumaa (02.08.2019) mjini Cologne, magharibi mwa Ujerumani, zimeishtua timu nzima ya Idhaa ya Kiswahili ya DW mjini Bonn.
Mohammed alikuwa mwandishi habari mahiri katika nyanja zote, lakini alipendelea sana taarifa ya habari za ulimwengu na makala ya mbiu ya mnyonge.

Asilimia kubwa ya wasikilizaji walizipenda sana makala zake kuhusu masuala ya haki za binadamu na sauti yake ya huruma. Aliwapa sauti wasiokuwa na saut, hakukata tamaa kuwatafuta watu muafaka wa kuwahoji na alikuwa makini sana katika kuhakikisha taarifa zake pamoja na makala haziegemei upande mmoja.

Kama mwandishi, Mohammed alikuwa mfano wa kuigwa kwa wengi wetu. Amekuwa akiugua kwa kipindi cha takriban miaka miwili na muda wote huu hakuweza kufanya kazi. Hata hivyo hatukukata tamaa kwamba angepata afueni na kurejea kazini kujumuika nasi kuendelea na majukumu yake.

Katika wakati huu mgumu wa majaribu, fikra na dua zetu tunazielekeza kwa mke wake, binti yake na familia yake visiwani Zanzibar na ughaibuni. Tunawapa pole na kutoa rambirambi zetu kwa majonzi makubwa, machozi yakitiririka machoni mwetu. Tunawaombea. Tulimpenda, lakini Mungu amempenda zaidi.

Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya DW, Andrea Schmidt, na wafanyakazi wote wa idhaa hii mjini Bonn tunawapa pole jamaa, marafiki na mashabiki kwa kuondokewa na mpendwa wetu.
 
Skywalker mmemuacha wapi? Jamaa akianza kuhadithia kitu lazima uendelee kumsikiliza tu
 
Nimefuatilia sana kwenye radio na mitandaoni pia nimegundua kuna watu wako vizuri sana kwenye usomaji wa makala. Top 3 yangu hii

3. Spesho Kabwanga (kituo chake youtube) anasomaga pia kwenye sports extra.

2. Ananias Edgar Makaza zake nyingi nazipataga youtube nimemjulia huko.

1. Mtiga Abdala. Huyu nimemjua kwenye the story book ya wasafi fm.

Hata makala iwe mbovu usomaji wao tu utaipenda.
Nawakublia sana hebu ongeza mwingine unaemjua nimtafute

Yupi kati ya hao Watatu pengine ungependa Siku moja aje Kukuchumbia na ikiwezekana afunge kabisa Pingu za Maisha ya Milele Daima nawe?
 
Yupi kati ya hao Watatu pengine ungependa Siku moja aje Kukuchumbia na ikiwezekana afunge kabisa Pingu za Maisha ya Milele Daima nawe?
Duuuh jf ya siku izi!
 
Kareja Kaunda. VORSA. huyu nilimkubali sana na bado namkubali
 
Back
Top Bottom