Familia ilipata nyumba kwenye flats, wakijaliwa watoto watoto wawili, baba alipata mchepuko kwenye flats zile zile ni mdada mwenye career yake lakini yuko single.
Yaani usiku mwaume akiona tu taa za dada zinawaka ana shuka chini anakaa mpaka muda wa kulala ndiyo anapanda juu kwa mkewe.
Mapenzi yalivyomkolea alikuwa anapika chakula akitoka kazini na kumshushia mchepuko anapokwenda.
Stori nzima niliipata church mrs alipotoa ushuhuda jinsi shetani alivyotaka kuvunja ndoa yake, ndipo nilipowaza huyu mwanaume si ajabu hata kuoga hakuwa anawahi katika kusave muda.