MWANAMUZIKI ambaye alishirikishwa kwenye Wimbo wa Nitarejea ya mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Hawa Said hali yake imezidi kuwa mbaya baada ya kulazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar akisumbulia na tatizo la ini.
Akizungumza na Ijumaa, mmiliki wa kituo cha kudhibiti matumizi ya madawa ya kulevya cha Pilli Missana Foundation, kilichopo Kigamboni jijini Dar, Pilli Missana alisema kuwa, tatizo la Hawa limetokana na matumizi ya madawa ya kulevya alilokuwa akichanganya na unywaji wa pombe kali.
“Unajua Hawa hali yake ilishaanza kutengamaa kabisa lakini kumbe alikuwa amepata tatizo la ini muda mrefu kutokana na unywaji wa pombe kali, kwa sasa hali yake si nzuri sana na anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Muhimbili,” alisema Pilli.
Julai mwaka jana, Hawa alijitokeza hadharani na kuomba msaada baada ya kuathiriwa na unywaji wa pombe kali za kienyeji pamoja na madawa ya kulevya ambapo alipatiwa msaada na Kituo cha Pilli Missana na hali yake kuanza kuimarika kabla ya kupata tatizo jingine la ini.
Huu ndo wimbo alishirikiana na Diamond
NITAREJEA by Diamond Platnumz ft Hawa
Aah vipi mizigo umesha weka tayari mh aah sijechelewa nikaja achwa na gari mh aah
Basi jikaze usilie mpenzi aah mi nitarudi niombee kwa Mwenyezi aah
Zile taabu na njaa msimu mzima mavuno hakuna hua nakosa raha pale mkikosa cha kutafuna
Roho yangu inauma sema nitafanya nini na pesa sina nakuonea na huruma bora niende mjini kusaka tumaa
Kama watoto wakinililia waambie kesho nitarejea wadanganye na vibagia waambie pipi nitawaletea
Kama watoto wakinililia waambie kesho nitarejea na usichoke kuvumilia na kila siku kuniombea
Wewe unajua kwamba nafsi na roho vitakuwa na wasiwasi upweke na moyo utajawa na simanzi
Nitapo kuwa nakwenda shambani alafu niko peke yangu honey nitapo kuja kuwa na majirani nitaumia aah
Pale ninapotoka kisimani ama nipo na kuni kichwani sina wa kunitua nyumbani nitalia
Maneno yako yananifanya nakosa raha na mawazo hata mwenzako sijawahi kufika Dar huu ndo mwanzo
Vile nakwenda na sijui pa kukaa wala mavazi ooh we niombee niepushwe na balaa na maradhi ooh eeh
Kama watoto wakinililia waambie kesho nitarejea wadanganye na vibagia waambie pipi nitawaletea
Kama watoto wakinililia waambie kesho nitarejea na usichoke kuvumilia na kila siku kuniombea
Unapokwenda kama ukifika salama utukumbuke na sisi usisahau kwaba mkeo na wana umetuacha na dhiki
Hilo usijali ila naomba chunga sana ogopa na marafiki wakikulagai hata kwa mbegu za mtama waambie sidanganyiki
Unapokwenda kama ukifika salama utukumbuke na sisi kumbuka mkeo nyumbani na wana umetuacha na dhiki
Hilo usijali ila naomba chunga sana ogopa na marafiki wakikulagai hata kwa mbegu za mtama waambie sidanganyiki eeeh eeeh oooh nitarejea mama niombee nirudi salama oooh watoto wadanganye iih uuh uuh aah tozalee zijaee hmm kamaaa…
Kama watoto wakinililia waambie kesho nitarejea (nitarejea mama) wadanganye (uuh wadanganyee) na vibagia waambie pipi nitawaletea
Kama watoto wakinililia (kamaa)waambie kesho nitarejea (nitarejea mama) na usichoke kuvumilia (usichoke) na kila siku kuniombea (nirudi salama)