Hawa Nitarejea wa Diamond yupo hoi kitandani, anaomba msaada wa kusaidiwa

Hawa Nitarejea wa Diamond yupo hoi kitandani, anaomba msaada wa kusaidiwa

Two dimension array

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2018
Posts
1,592
Reaction score
2,381

MWANAMUZIKI ambaye alishirikishwa kwenye Wimbo wa Nitarejea ya mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Hawa Said hali yake imezidi kuwa mbaya baada ya kulazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar akisumbulia na tatizo la ini.

Akizungumza na Ijumaa, mmiliki wa kituo cha kudhibiti matumizi ya madawa ya kulevya cha Pilli Missana Foundation, kilichopo Kigamboni jijini Dar, Pilli Missana alisema kuwa, tatizo la Hawa limetokana na matumizi ya madawa ya kulevya alilokuwa akichanganya na unywaji wa pombe kali.

“Unajua Hawa hali yake ilishaanza kutengamaa kabisa lakini kumbe alikuwa amepata tatizo la ini muda mrefu kutokana na unywaji wa pombe kali, kwa sasa hali yake si nzuri sana na anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Muhimbili,” alisema Pilli.

Julai mwaka jana, Hawa alijitokeza hadharani na kuomba msaada baada ya kuathiriwa na unywaji wa pombe kali za kienyeji pamoja na madawa ya kulevya ambapo alipatiwa msaada na Kituo cha Pilli Missana na hali yake kuanza kuimarika kabla ya kupata tatizo jingine la ini.
 
Jamani kama kuna mtu ana connection na wale Lions club afanye kuwasiliana nao huyu demu apelekwe India nakumbuka kuna demu mmoja miaka ileee alipelekwa akapona
 
My God!
Pole sana. Ila sasa kama kila demu aliyepitiwa na diamond atatajwa kuwasaidia si watajaa mkoa mzima jamani ataweza kweli!
Kwa mujibu wa huyo binti, alisema waliishi na anayejiita Diamond kama MKE na MUME mpaka hapo jamaa alipojikusanyia umaarufu usio na manufaa. Mama wa jamaa anadaiwa aliutambua na kuunga mkono uhusiano ule
 
Duh so aweza kuwa chanzo cha yeye kuwa hivyo
Stress na
Depression zilimdumbukiza kwenye madawa hence figo kufeli break
 
Duh so aweza kuwa chanzo cha yeye kuwa hivyo
Stress na
Depression zilimdumbukiza kwenye madawa hence figo kufeli break
Alisema anatumia poda na machozi ya simba haswaaaa......machozi ya simba inaweza kuwa sababu kubwa
 
MWANAMUZIKI ambaye alishirikishwa kwenye Wimbo wa Nitarejea ya mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Hawa Said hali yake imezidi kuwa mbaya baada ya kulazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar akisumbulia na tatizo la ini.

Akizungumza na Ijumaa, mmiliki wa kituo cha kudhibiti matumizi ya madawa ya kulevya cha Pilli Missana Foundation, kilichopo Kigamboni jijini Dar, Pilli Missana alisema kuwa, tatizo la Hawa limetokana na matumizi ya madawa ya kulevya alilokuwa akichanganya na unywaji wa pombe kali.

“Unajua Hawa hali yake ilishaanza kutengamaa kabisa lakini kumbe alikuwa amepata tatizo la ini muda mrefu kutokana na unywaji wa pombe kali, kwa sasa hali yake si nzuri sana na anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Muhimbili,” alisema Pilli.

Julai mwaka jana, Hawa alijitokeza hadharani na kuomba msaada baada ya kuathiriwa na unywaji wa pombe kali za kienyeji pamoja na madawa ya kulevya ambapo alipatiwa msaada na Kituo cha Pilli Missana na hali yake kuanza kuimarika kabla ya kupata tatizo jingine la ini.

Huu ndo wimbo alishirikiana na Diamond

NITAREJEA by Diamond Platnumz ft Hawa
Aah vipi mizigo umesha weka tayari mh aah sijechelewa nikaja achwa na gari mh aah
Basi jikaze usilie mpenzi aah mi nitarudi niombee kwa Mwenyezi aah
Zile taabu na njaa msimu mzima mavuno hakuna hua nakosa raha pale mkikosa cha kutafuna
Roho yangu inauma sema nitafanya nini na pesa sina nakuonea na huruma bora niende mjini kusaka tumaa

Kama watoto wakinililia waambie kesho nitarejea wadanganye na vibagia waambie pipi nitawaletea
Kama watoto wakinililia waambie kesho nitarejea na usichoke kuvumilia na kila siku kuniombea

Wewe unajua kwamba nafsi na roho vitakuwa na wasiwasi upweke na moyo utajawa na simanzi
Nitapo kuwa nakwenda shambani alafu niko peke yangu honey nitapo kuja kuwa na majirani nitaumia aah
Pale ninapotoka kisimani ama nipo na kuni kichwani sina wa kunitua nyumbani nitalia

Maneno yako yananifanya nakosa raha na mawazo hata mwenzako sijawahi kufika Dar huu ndo mwanzo
Vile nakwenda na sijui pa kukaa wala mavazi ooh we niombee niepushwe na balaa na maradhi ooh eeh

Kama watoto wakinililia waambie kesho nitarejea wadanganye na vibagia waambie pipi nitawaletea
Kama watoto wakinililia waambie kesho nitarejea na usichoke kuvumilia na kila siku kuniombea

Unapokwenda kama ukifika salama utukumbuke na sisi usisahau kwaba mkeo na wana umetuacha na dhiki
Hilo usijali ila naomba chunga sana ogopa na marafiki wakikulagai hata kwa mbegu za mtama waambie sidanganyiki

Unapokwenda kama ukifika salama utukumbuke na sisi kumbuka mkeo nyumbani na wana umetuacha na dhiki
Hilo usijali ila naomba chunga sana ogopa na marafiki wakikulagai hata kwa mbegu za mtama waambie sidanganyiki eeeh eeeh oooh nitarejea mama niombee nirudi salama oooh watoto wadanganye iih uuh uuh aah tozalee zijaee hmm kamaaa…

Kama watoto wakinililia waambie kesho nitarejea (nitarejea mama) wadanganye (uuh wadanganyee) na vibagia waambie pipi nitawaletea

Kama watoto wakinililia (kamaa)waambie kesho nitarejea (nitarejea mama) na usichoke kuvumilia (usichoke) na kila siku kuniombea (nirudi salama)
 
Si ndo alisema eti Mondii alimwambia wakarare bahalini siku saba wapate pesa za manjini..
 
Back
Top Bottom