niachiemimi
JF-Expert Member
- Feb 18, 2015
- 3,606
- 5,295
Shoka linalochagua mti wa kukata hilo siyo shoka. Sema awe mstarabu anamopita maana kesho haya yanayowakuta alioenda nao yaweza kumkuta pia.Ila diamond jamani hachaguagi kuuma
Sasa mbona mpira unaurusha kwingine?huu wa kwetu sote..Masikini hii dunia hii[emoji24] [emoji24] .....Dai umeona hii??
Pole sana Hawa
[emoji3][emoji3] kuna nini mkuuWasimpeleke ic-yu
Mtoa roho kapiga kambi huko! Wamemrahisishia kazi yake.[emoji3][emoji3] kuna nini mkuu
Ila mama yake kanihudhunisha sana. Umaskini ni mbaya sana.Mtoa roho kapiga kambi huko! Wamemrahisishia kazi yake.
Hawa wapuuzi hawastahilo huruma, huu ni wakati wa kila mtu kupambana na hali yake, pesa za kubwia unga kama nyoka angelipia bima ya NHIF saa hizi asingetuletea huu upuuzi wake.
Tena hii tabia ikome.
Kafanya nini mkuu huyo maza!Ila mama yake kanihudhunisha sana. Umaskini ni mbaya sana.
Maza analia sana mwanawe apate msaada wa matibabu.Kafanya nini mkuu huyo maza!
Ni huzuni kwa kweli! Huyo amenisikitisha zaidi kwa maumivu anayoyapata mwanae ni kiasi gani mama zetu wanapata maumivu wanaonapo watoto wao tupatapo majanga,huenda binti huyu angejituliza na kuishi maisha ayatakayo mola wake basi mama yake asingemwaga machozi leo hii kumlilia mwanae anavyopata tabu,tunaamini kila tatizo ni mpango wa Muumba lkn mengine ni shetani kupitia sisi,Na hatua iliyofikia kwa mgonjwa ni matumaini yake ya kupandikizwa ini tena huduma ambayo haijulikani itaanza lini na elimu yangu ndogo ini ni moja kupandikizwa sijui itang'olewa ya nani ili apone,mwenye kuweza hilo ni mama anaeumia leo kwa matatizo aliyomkanya mtoto jana,Hatua iliyopo kwa mgonjwa ni mbaya na anapata taabu sana tumuombee tu " Kama Mwenyezi Mungu alimpa uhai zaidi ya alionao sasa basi na ampe nafuu na kumponya mjawake huyu ila kama ni muda umefika basi na amchukue kumpoza na maumivu ayapatayo leo"tunamuombea kheri ktk tiba yake,kupona kwake,na kumlejea mola wake.
MWANAMUZIKI ambaye alishirikishwa kwenye Wimbo wa Nitarejea ya mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Hawa Said hali yake imezidi kuwa mbaya baada ya kulazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar akisumbulia na tatizo la ini.
Akizungumza na Ijumaa, mmiliki wa kituo cha kudhibiti matumizi ya madawa ya kulevya cha Pilli Missana Foundation, kilichopo Kigamboni jijini Dar, Pilli Missana alisema kuwa, tatizo la Hawa limetokana na matumizi ya madawa ya kulevya alilokuwa akichanganya na unywaji wa pombe kali.
“Unajua Hawa hali yake ilishaanza kutengamaa kabisa lakini kumbe alikuwa amepata tatizo la ini muda mrefu kutokana na unywaji wa pombe kali, kwa sasa hali yake si nzuri sana na anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Muhimbili,” alisema Pilli.
Julai mwaka jana, Hawa alijitokeza hadharani na kuomba msaada baada ya kuathiriwa na unywaji wa pombe kali za kienyeji pamoja na madawa ya kulevya ambapo alipatiwa msaada na Kituo cha Pilli Missana na hali yake kuanza kuimarika kabla ya kupata tatizo jingine la ini.