Hawa Nitarejea wa Diamond yupo hoi kitandani, anaomba msaada wa kusaidiwa

Hawa Nitarejea wa Diamond yupo hoi kitandani, anaomba msaada wa kusaidiwa

Umefikia hatua ya kuvuna alichokipanda kwenye unywaji wa gonga na madawa ya kulevya.
Kwa tumbo hili, mti hapigwi, pombe hanywi na madawa ya kulevya hatumii.
 
Ndiyo yale yale.
Wakiwa safi Pesa hadi mitandaoni wanapiga selfie nazo ili tuwaone walivyo mambo safi.

Ila wakiugua wanatembeza bakuli.

Pole sana Hawa
 
Wapi yule Nyerere mfupi, mkiti wa kudumu wa misiba, jitokeze hadharani. Onyesha juhudi au ww huangaiki na walio hai.
 


MWANAMUZIKI ambaye alishirikishwa kwenye Wimbo wa Nitarejea ya mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Hawa Said hali yake imezidi kuwa mbaya baada ya kulazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar akisumbulia na tatizo la ini.

Akizungumza na Ijumaa, mmiliki wa kituo cha kudhibiti matumizi ya madawa ya kulevya cha Pilli Missana Foundation, kilichopo Kigamboni jijini Dar, Pilli Missana alisema kuwa, tatizo la Hawa limetokana na matumizi ya madawa ya kulevya alilokuwa akichanganya na unywaji wa pombe kali.

“Unajua Hawa hali yake ilishaanza kutengamaa kabisa lakini kumbe alikuwa amepata tatizo la ini muda mrefu kutokana na unywaji wa pombe kali, kwa sasa hali yake si nzuri sana na anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Muhimbili,” alisema Pilli.

Julai mwaka jana, Hawa alijitokeza hadharani na kuomba msaada baada ya kuathiriwa na unywaji wa pombe kali za kienyeji pamoja na madawa ya kulevya ambapo alipatiwa msaada na Kituo cha Pilli Missana na hali yake kuanza kuimarika kabla ya kupata tatizo jingine la ini.
Ni huzuni kwa kweli! Huyo amenisikitisha zaidi kwa maumivu anayoyapata mwanae ni kiasi gani mama zetu wanapata maumivu wanaonapo watoto wao tupatapo majanga,huenda binti huyu angejituliza na kuishi maisha ayatakayo mola wake basi mama yake asingemwaga machozi leo hii kumlilia mwanae anavyopata tabu,tunaamini kila tatizo ni mpango wa Muumba lkn mengine ni shetani kupitia sisi,Na hatua iliyofikia kwa mgonjwa ni matumaini yake ya kupandikizwa ini tena huduma ambayo haijulikani itaanza lini na elimu yangu ndogo ini ni moja kupandikizwa sijui itang'olewa ya nani ili apone,mwenye kuweza hilo ni mama anaeumia leo kwa matatizo aliyomkanya mtoto jana,Hatua iliyopo kwa mgonjwa ni mbaya na anapata taabu sana tumuombee tu " Kama Mwenyezi Mungu alimpa uhai zaidi ya alionao sasa basi na ampe nafuu na kumponya mjawake huyu ila kama ni muda umefika basi na amchukue kumpoza na maumivu ayapatayo leo"tunamuombea kheri ktk tiba yake,kupona kwake,na kumlejea mola wake.
 
Back
Top Bottom