Hawa Nitarejea wa Diamond yupo hoi kitandani, anaomba msaada wa kusaidiwa

Kama una uwezo wa kumsaidia…..Msaidie akipona ndo uje kumsimanga.
 
Huo wimbo ndio uliomtambulisha sana Diamond ktk soko/ulimwengu wa bongo flavours kwanini jamaa asijitoe kwa hili akapata baraka kwa Mungu na kujiongezea washabiki? Hii ni fursa kwake japo ugonjwa hauna mwentewe.
 
unapojikuta katika kipindi kigumu..mfano depression,ugumu wa maisha.tulia.tumia busara kufikiri ni vipi utatoka au kucope hiyo hali..na kabla hujaamua kujiingiza katika maamuzi jiulize yatakupa matokeo gani? mazuri na mabaya yake,yapime uzito kisha jishauri niingie au la
hawa alipata anguko kama msanii.diamond akamuacha,akaamua kudate na mwanaume mwingine nae akampachika mimba akaikataa.maamuzi yake ya kujiingiza kwenye madawa ya kulevya na kunywa gongo tena akiwa na mimba faida yake ni ndogo kuliko madhara.
Mungu atampigania
 
Kumuombea kwa Mungu ni msaada tosha, maana yeye ndiye hakimu.
nadhani haukumfahamu vizuri huyu dogo kabla hajaanza kuumwa ndio maana unasema hivyo.
Kama Mungu ndo hakimu…….mbona una onekana kumuhukumu kwa matendo yake ya nyuma….. Ww kumjua zaidi hakumsaidii kutoka kwenye matatizo yake.
 
Kama Mungu ndo hakimu…….mbona una onekana kumuhukumu kwa matendo yake ya nyuma….. Ww kumjua zaidi hakumsaidii kutoka kwenye matatizo yake.
Ningekuwa nimemhukumu, nisingemuombea hata hiyo huruma ya Mungu. Ninge'conclude kwa kusema hafai kusaidiwa ova.
Ila badala yake sijashawishi mtu alimsaidie, ila mimi sitaweza kumsaidia kwa hata 100 mbovu na kumwachia Mungu
 
Nawaomba wasanii kwa umoja wetu tumchangie msanii mwenzetu bi hawa anaumwa Ini limevimba.Msanii huyu ndie yule aliyeimba na Msanii Diamond wimbo uitwao Nitarejea .Msanii Hawa amelazwa Hospital ya Muhimbili
Kama binadamu wengine wakiwa kwenye shida tunaweza kumchangia/kuchangiwa....ila tujiulize Kuna watu wangapi wenye shida Kama yake wapo hospitali na hakuna mtu wa kuwasemea. Besides Hawa wasanii na watu mashuhuri wanapopata shida wanakuwa wa kwanza kuja mitandaoni kuomba msaada wa matibabu lakini wanapokuwa wazima huwa hawarudishi fadhila kwa kusaidia wenye shida na wamekuwa wakiishi maisha ya anasa Sana na kujionyesha kuwa Wana hela...tujifunze juu ya haya japo hayo niliyoyaeleza hayaondoi sababu ya kumsaidia
 
siwezi kumchangia msanii hata siku moja ndo hao hao wakipona wanaanza kujiita the boss lady
Na kutuita wengine Low life! Wengine wako segerea kwa kuzidhalilisha fedha na wengine wapo hospital wanasubiria huruma za Mungu kwa kuwa hawana fedha hata za matibabu,na wote eti ni ma celebrity!
 
GONGO???
 
Kwa mujibu wa huyo binti, alisema waliishi na anayejiita Diamond kama MKE na MUME mpaka hapo jamaa alipojikusanyia umaarufu usio na manufaa. Mama wa jamaa anadaiwa aliutambua na kuunga mkono uhusiano ule
Unaweza kukuta hiyo ndio sababu kuu inayo mfanya kunywa pombe kupita kiasi
 
Hawa wapuuzi hawastahilo huruma, huu ni wakati wa kila mtu kupambana na hali yake, pesa za kubwia unga kama nyoka angelipia bima ya NHIF saa hizi asingetuletea huu upuuzi wake.
Tena hii tabia ikome.
Aiseeee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…