Hawa Nitarejea wa Diamond yupo hoi kitandani, anaomba msaada wa kusaidiwa

Hawa Nitarejea wa Diamond yupo hoi kitandani, anaomba msaada wa kusaidiwa

View attachment 879865 View attachment 879867

Hawa wa 'Diamond' msanii wa Bongo fleva aliyeimba na msanii maarufu Diamond Platnumz wimbo wa Nitarejea kwasasa anahitaji msaada wa hali na mali kutokana na hali yeke ya kaifya kwa sasa,Akihojiwa na kipindi cha Shelawadu Hawa akiwa nyumbani na mama yake alionekana akiwa katika maumivu makali sana huku akionekana akiwa na tumbo kubwa sana na alipohojiwa na mtangazaji w akipindi hicho alisema amaekuwa akipata matibabu yake katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa kutolewa maji kila yanapojaa na hakuna lingine zaidi ya hilo na alipohojiwa zaidi alisema kuwa ameambiwa ini lake ni kubwa na halifanyi kazi vizuri hivyo atakuwa anatolewa maji tu ingawa anasema kuwa aliuliza kama kuna tiba nyingine akaambiwa ni kubadili ini na kuweka ini lingine lakini kwasasa huduma hiyo haitolewi Muhimbili labda mpaka mwakani.

Nadhani wengi wamesaidiwa na wadau au serikali kwa sababu sauti zao zilisikika na wenye mamlaka mfano mzuri ni Wastara sasa na huyu ni msanii na mtanzania ambaye naye anahitaji msaada wa hali na mali hasa msaada wa tiba na inavyoonekana kwasasa ni tiba ya ini au kubadili ini yaan Liver transplant kazi ambayo haifanyiki Tanzania mpaka huko nje ya nchi.
Nadhani wadau wanaohusika ni muhimu sasa kuangalia jinsi ya kumsaidia huyu dada ambaye anaangamia taratibu huku akiona kama sasa mwisho wa maisha yake umefika kama kuna uwezekana wa kufanya jambo kwa binti huyu basi tufanye sasa ili kuokoa maisha yake.
Hadi huruma
 
ETI
"Hali yake imezidi kuwa mbaya baada ya kulazwa...."
cha ajabu ni kuwa wachangiaji woote wamepigwa na upofu!!!
 
Kwa mujibu wa huyo binti, alisema waliishi na anayejiita Diamond kama MKE na MUME mpaka hapo jamaa alipojikusanyia umaarufu usio na manufaa. Mama wa jamaa anadaiwa aliutambua na kuunga mkono uhusiano ule
Inasemekana chanzo cha wao kuachana ni baada ya Dai kugundua mwenza wake ni mlevi pia alikua akivuta poda
 
Haya maisha ya dunia hii ni mtihani mkubwa sana ,Nyimbo pekee ya Diamond ninayoipenda ni hii Nitarejea ,Pole Hawa
 
Back
Top Bottom