
Na Haruni Sanchawa
Bosi wa Tanzania Awamu ya Tatu, Benjamin William Mkapa amewabana mahausigeli na mahausiboi akitaka wasipewe ajira bila kuwa na mafaili yenye rekodi inayoonesha maeneo wanayoweza kupatikana punde wanapoharibu kwa waajiri wao na kuingia mitini.... Mheshimiwa Mkapa aliyasema hayo Jumatano iliyopita, kwenye msiba kwa Balozi Mstaafu, Andrew Daraja ambapo shambaboi, James Maburu anatuhumiwa kumuua kwa kumchoma na kisu mke wa balozi huyo.
Akiongea katika hali ya masikitiko na majonzi mazito wakati akiagana na baadhi ya waombolezaji, Mkapa alisema iko haja kwa waajiri wa wafanyakazi wa ndani kuhakikisha kila anayeajiriwa (hausigeli, hausiboi) anafunguliwa ‘faili' lenye vielelezo vyote vitakavyowezesha kupatikana kwake punde inapotokea anafanya uhalifu na kukimbia.