Hawa Tala Tanzania ninyi mnawaelewa?

genius_

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2018
Posts
474
Reaction score
1,237
"Tala ni app nambari 1 Tanzania inayotoa huduma za kifedha kwa wadau wanaotumia mtandao wa Tigo na Vodacom !

Tunakupatia mkopo mikononi mwako, wakati wowote na mahali popote. Pia ada zetu ni ndogo na tuna ratiba rahisi za marejesho.

Je! Inafanyaje kazi?
- Fungua akaunti yako ya Tala
- Omba mkopo kwa dakika 5 tu
- Pata jibu la ombi lako la mkopo baada ya sekunde chache tu
- Pesa itatumwa papo hapo kwenye akaunti yako ya Tigo Pesa au M-PESA
- Kopa na rejesha mkopo kwa wakati uweze kukopa viwango vikubwa zaidi

Sera ya Faragha: Unapo-download programu ya Tala, tutakuomba kusoma SMS zako pamoja na taarifa nyingine ili kuhakiki utambulisho wako, na hali yako ya kifedha, ili tuweze kukupatia mkopo wa haraka popote ulipo Tanzania. Tunathamini sana faragha na taarifa zako binafsi hazitatolewa kwingine bila ya wewe kutoa idhini."

ndugu wana Jf naomba ushuhuda wa watu waliopata mkopo kupitia hawa watu, na je kuhusu hiyo sera yao ya faragha haiwezi kutumika vibaya hasa wanapopata taarifa za mtu husika?

msaada tafadhali vyuma vimekaza[emoji16] [emoji16]
 
Mm ni mmoja kati ya watu wanaofaidika na mkopo toka tala, hawana shida hawana usumbufu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Write your reply...mimi mpk ss wananidai 275000 ukifata mashart wako vzr
hapo kwenye sera ya faragha(privacy) ndo panaponipa mashaka, ni kweli kuwa wanasoma msg zako ili kupata uhakika wa kukuamini ndipo wakukopeshe hiyo pesa?
 
Ata Mimi pia tena nipo ktk kiwango kikubwa ktk ukopaji.walinipigia cm kunipa pongezi kwa kua mkopaji wa mda mrefu.

Sent using Jamii Forums mobile app
hongera ndugu..ushuhuda mzuri ila nahitaji kufahamu itanichukua mda gani mpk kupata huo mkopo baada ya kufata procedures zote
 
Hawana SHIDA..lengo lao kukuchek KWELI unachoomba unamaanisha? ndy maana unaulizwa SABABU YA KUKOPA,,,,na wanachek TIGO PESA ,AU VODA PESA YAKO IPO VZR? Au ndy wake TUMA KWENYE NAMBA HII...ila hawana shida,,wapo vzr sn tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilijaribu Mara moja kuwakopa..mbwa sana wale unalipa deni unaongezewa 10000 ambayo ukija kukopa tena unajikuta umewafaidisha wao wewe wamekukopa 4000...wizi tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli kabisaaa kuna siku nlilipa mkopo wa 72 elfu nikakopeshwa elfu 70 ....sijalipa mpaka kesho na silipi mpaka kiama wajinga sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hapo kwenye sera ya faragha(privacy) ndo panaponipa mashaka, ni kweli kuwa wanasoma msg zako ili kupata uhakika wa kukuamini ndipo wakukopeshe hiyo pesa?
Hakunaaaa we jisajiri chukua kitambulisho weka detail pale jibu maswali chapuuuu unapewa mkopo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo tala kwenye kujisajiri mnaitaji marekebisho mnataka mtu awe na kitambulisho cha kira pekee badala ya vitambulisho vyote muhimu kama cha taifa na chakupigia kula wengi tunashindwa kutumia huduma hii kwakua hatuna vitambulisho vya kula,ebu jirekebisheni hapo tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…