Hawa Traffic wa Njiro wamezidi kupokea rushwa!

Hawa Traffic wa Njiro wamezidi kupokea rushwa!

siyabonga

Senior Member
Joined
Jan 25, 2012
Posts
125
Reaction score
35
Wakuu, kiwavi hiki cha utawala mbaya na rushwa katika Jeshi hili kitaisha lini?

Mfano, hawa traffic wa barabara ya kwenda Njiro, Arusha, wanasimama katikati kabisa ya bara bara, kila gari lazima wasimamishe na kuomba rushwa bila aibu! Why?

Hawana kazi nyingine za kufanya au njia ya kiakili zaidi ya kutekeleza majukumu yao? Mfano, kutoa elimu ya usalama barabarani mashuleni na vyuoni?
 
kazi nyingine ya kufanya kama wangepata hiyo nafasi kupiga watu mabomu ya machozi, risasi za moto, na maji washawasha. kama hawajapangiwa kufanya hivyo iliyobaki ni rushwa
 
Wakikuomba rushwa waambie wakupe namba yao ya simu na uwatumie rushwa iyo kwa tigo pesa\m-pesa alafu tutaanzia kesi hapo.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Natamani tumkodi Kagame kwa miezi mitatu tu ujinga huu hutauona!
 
Back
Top Bottom