DOKEZO Hawa Trafiki wanakera sana, njaa zitawaua

DOKEZO Hawa Trafiki wanakera sana, njaa zitawaua

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

kimsboy

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2016
Posts
9,846
Reaction score
20,319
Hakuna kitu kinakera kama kila saa na kila siku unakamatwa na traffic hata kama huna kosa watakutafutia visababu.

Hawa jamaa ni watu wa hovyo sana, ndo maana huishia kufa masikini, kinachowatesa ni njaa zao, wivu na roho mbaya dhidi ya wenye magari, kwani kuna mtu aliwatuma wafanye kazi za kuchomwa na jua, ingekua hata wanamiliki magari walau basi.

Kila siku mnasababisha foleni, hawa ndo wanahusika na kusababisha foleni maeneo mengi hapa Dsm mfano nzuri ni pale Buguruni na Mwenge.

Hivi hawa jamaa wanadhani wenye magari ni matajiri sana wa kuwakamua? Karibia kila wiki hela inanitoka mara tatu mara nne.

Tuna taifa la hovyo sana lenye askari wa hovyo wa usalama barabarani.

Hovyo kabisa!
 
Kuwategemea kina Kinana kuamka vizuri siku moja moja si la kulalia mlango wazi

IMG_20220911_074706_842.jpg
 
Pole mkuu hao ndio walivyo PRA Polisi Revenue Authority, vumilia tu maana hatuna kwa kwenda ukilalamika sana unaambiwa hamia Burundi.
 
Hao rushwa ipo ndani ya damu zao.
Wanatafuta pesa za kuhonga na kulewea.
 
Wanakera wanafosi kukutafutia kosa hata kama ni la uongo ilimradi wakupige hela
 
Halafu wakiondolewa hata mtu akidondoka na baiskeli utasikia wanasema, si hawaoni umuhimu wetu
 
Umepigwa faini ngapi? Ukapata hasira ya kuja jamii forum kutoa ya moyoni.

Polee
 
Back
Top Bottom