Hawa vijana wa Bongofleva walipotelea wapi?

Hawa vijana wa Bongofleva walipotelea wapi?

incredible terminator

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2016
Posts
2,498
Reaction score
4,162
Hawa Vijana hata social network zao haziko Active kabisa kuonesha hawataki hata kujihusisha na mambo ya kisanaa na kijamii,


Ninachojua ni kwamba walikuwa vijana wanajitahidi sana ila Gafla walizima kama taa wala hakuna sehem wanaongelewa au kujiongelea kwenyewe.

1.FUTURE JNL,

Huyu kijana alikuwa machachali sana kwenye machupa makali na sauti kali sana, Swaga za kibraza men na bata za kutosha. Alitamba na Ngomaa kama Kubali, Tena, Visiwani, mara ya mwisho alikuwa anamilikiwa na boss tajiri Petman Rasta.

2. HERI MZIKI.

Huyu ni kijana machachali ambae alitamba na ngoma ya sweetlove, kijana barobaro ambae baadae alianza kuhusika kulelewa na kutoka kimapenzi na mwanadada mwenye sauti ya kutoa nyoka pangoni Mtangazaji mchachali ambae kwa kijana huyu tulimuona kama Mshangazi ambae ki umri walikuwa hawaendani na kijana, Mtangazaji Diva the bowse, kipindi hiko bado alikuwa Clouds media.

3. MAYUNGA.

Huyu ni kijana ambae alibahatika kupiga collable na msanii mkubwa Akon hata kabla ya mastaa mnaowajua nyie hawajafanikiwa kutoa ngoma na wasanii wakubwa wa Internation ila dogo alipenyeza kuwa mshindi wa Shindano lililoandaliwa na Aitel kusaka vipaji Afrika na hapa ndio tukampata mwamba kutoka Morogoro mwenye asili ya Tabora msukuma flani ivi Blazamen akabeba kijiti

Mwamba, na hapo alibahatika kufanya pini na Msanii Akon ngona ya Don't go away huku Video quuen wa ngoma hiyo inasemekana ni mwanadada ambae alishawahi kufanya chupa ya Chris brown (Breezy) mwamba alitisha sana ila baada ya ushindi mwamba katokomea alikotokomea.

4 DAVY STAR (DAVISTA)
Huyu alikuwa bwana mdogo tokea pande za mwanza, Hakupata umaarufu kiivo ila ngoma lake moja ilipenya sana kwa pande za kanda ya ziwa kutokana kwamba alimshirikisha mkali mo music ambae kwa miaka ile alikuwa katika form hivyo alifanya Goma lipenye kwa uharaka lakini pia chupa lilikaa kinyamwezi sana Enzi hizo

Hanscana alikuwa hajaharibiwa nyota na Nabii Kiboko ya Wachawi wa Buza. Dogo kwa tetesi alikuwa anasomea Urubani chuo × huko Durbun kwa madiba, na baada ya hilo Goma dogo alitoa magoma mengine kadhaa ila hayakwenda na hatmae alizima Gafla hata kwenye social networks.

5. COYO MC

Huyu alikuwa mwamba flani ivi toka pande za Mwanza alitamba kwa miondoko flan ya Hip hop dance, wengi wanaita commacial miondoko flani ivi ya Ki darasa SmG, Mwamba alitamba na pini kama vile "ziwafikie" na Itakucost na baada ya hapo mwamba kapata kichwa kiana, ni Rapa kutokea Mwanza ila kuna Interview moja nilmskia akisema hamjui Youngkiller licha ya kuwa wasanii wanaotokea mkoa mmoja, Mkolani na Mabatini Mwaza na baadae mwamba akatulia hadi sasa hajulikani alipo wala anafanya nini.

6.MIRROR RYMES.

Alikuwa bwana mdogo fundi sana alikuwa anasimamiwa na mwanadada Wema Sepetu, mwamba alitoka kwa ngoma moja tisha sana inaitwa "I give you my money" akiwa na mkali Cowbamma, Marehem Albert mangwea na zingine nyingi kama vile Koro, etc baadae mwamba alizima gafla na hakujulikana alienda wapi na hakuna sehem anazungumziwa.

MI NAWASILISHA KWA YOYOTE MWENYE TAARIFA ZA HAWA VIJANA AU MMOJA KATI YAO ANAKARIBISHWA ATUSAIDIE KUJUA VIJANA WAKO WAPI HAWA.
 
Huyo heri muziki ni kijana mwenye kipaji sana sana sijui alijichukulia poa tu.

Pia huyo mirror alichobugi ni kujiweka kwa wema sepetu.

Davista alikuwa one wonder hit
 
Yale mashart kama ya kina pididi ndo yaliwafanya wapotee kweny game .hata richmavoko naye yali mshinda🤐
 
Back
Top Bottom