Hawa vijana wanaovimba mtandaoni kwa maburungutu ya milioni 40 ni washamba wa pesa, Ili uvimbe kama don walau uringishie milioni 200

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Dar es salaam unakuta kijana ana coaster 10 na bado ukaonekana wa kawaida kabisa, ni tofauti na huko vijijini ama mikoani tayari umefika kipimo cha kuitwa tajiri.

Shida inakuja kwa hawa vijana wageni wa jiji wanatokea vijijini ama mikoani walikokuwa wanapata attention ya kuonekana ni matajiri, hawapati tena ile attention waliyoizoea, ndio hapo sasa jogoo la shamba linalazimisha kuwika mjini kwa kujirekodi mitandaoni.

Mtu anajisifu ni don kwa kuonyesha maburungutu ya milioni 30, anahisi bado yupo huko mikoani.

Vijana wenye kuweza kumudu milioni 50 hapa Dsm na hata Mwanza ni wengi si haba, hayo maburungutu ya 40 sio levo ya kuvimba.

Angalau uvimbe na dola laki 1 sawa na milioni 250 lakini hata ikiwa ni milioni 200 sio mbaya, milioni 40 ni za kuvimbia kijijini.
 
kiukweli scheni wavimbe tu maisha magumu street hata mi nkipata ata mil 5 lazm nivimbe maan sijawah kushika hata mil 1.4 yakwangu toka nizaLiwe
Masikini akipata matako hulia mbwata lakini hakikisha yanalia kwa usiri sio hadharani lasivyo utaonekana mshamba tu, hio milioni 5 unavimba lakini jua kuna vijana ni bajeti yao ya kila wiki kitambaa cheupe
 
Masikini akipata matako hulia mbwata lakini hakikisha yanalia kwa usiri sio hadharani lasivyo utaonekana mshamba tu, hio milioni 5 unavimba lakini jua kuna vijana ni bajeti yao ya kila wiki kitambaa cheupe
hayawezi kulia mbwata kila mtu ajue yatalia kimya kimya yaan jua kaLi bro kam mtu kaziotea achen avimbe ila sio kuvimba mpka kututukana tusio nacho
 
1. Cha mtu mavi
2. Bora ndege mmoja mkononi kuliko elfu mtini.

Ringa na chako hata kama buku
 
Raha sana kupiga picha hela
Hata kama ni za ada ya kina Junia 😁
Hata kama ni za rejeshoo
Hata kama huna pa kupost,, bakisha ukumbusho kwenye simu kwamba ulishikaga.

Ilaaaa
Watz na kupangia watu maisha tuna A+

#nisifokewe..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…