Hawa vijana wanaovimba mtandaoni kwa maburungutu ya milioni 40 ni washamba wa pesa, Ili uvimbe kama don walau uringishie milioni 200

Hawa vijana wanaovimba mtandaoni kwa maburungutu ya milioni 40 ni washamba wa pesa, Ili uvimbe kama don walau uringishie milioni 200

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Dar es salaam unakuta kijana ana coaster 10 na bado ukaonekana wa kawaida kabisa, ni tofauti na huko vijijini ama mikoani tayari umefika kipimo cha kuitwa tajiri.

Shida inakuja kwa hawa vijana wageni wa jiji wanatokea vijijini ama mikoani walikokuwa wanapata attention ya kuonekana ni matajiri, hawapati tena ile attention waliyoizoea, ndio hapo sasa jogoo la shamba linalazimisha kuwika mjini kwa kujirekodi mitandaoni.

Mtu anajisifu ni don kwa kuonyesha maburungutu ya milioni 30, anahisi bado yupo huko mikoani.

Vijana wenye kuweza kumudu milioni 50 hapa Dsm na hata Mwanza ni wengi si haba, hayo maburungutu ya 40 sio levo ya kuvimba.

Angalau uvimbe na dola laki 1 sawa na milioni 250 lakini hata ikiwa ni milioni 200 sio mbaya, milioni 40 ni za kuvimbia kijijini.
 
kiukweli scheni wavimbe tu maisha magumu street hata mi nkipata ata mil 5 lazm nivimbe maan sijawah kushika hata mil 1.4 yakwangu toka nizaLiwe
Masikini akipata matako hulia mbwata lakini hakikisha yanalia kwa usiri sio hadharani lasivyo utaonekana mshamba tu, hio milioni 5 unavimba lakini jua kuna vijana ni bajeti yao ya kila wiki kitambaa cheupe
 
Masikini akipata matako hulia mbwata lakini hakikisha yanalia kwa usiri sio hadharani lasivyo utaonekana mshamba tu, hio milioni 5 unavimba lakini jua kuna vijana ni bajeti yao ya kila wiki kitambaa cheupe
hayawezi kulia mbwata kila mtu ajue yatalia kimya kimya yaan jua kaLi bro kam mtu kaziotea achen avimbe ila sio kuvimba mpka kututukana tusio nacho
 
Unakusanya hela zako zinafika milioni 25 unaanza kujirekodi kwamba ni tajirii?

Nimekuja kugundua aina hii ya watu wanatokea vijijini ama mikoani ambako mtu ukiwa na milioni 50 unaonekana doni mtu mzito, sasa wakihamia kwenye jiji wanachukia hawapati ile attention ya vijijini, ndio hapo sasa jogoo la shamba linalazimisha kuwika mjini kwa kujirekodi.


Nashangaa kuona mtu anajisifu ana pesa kisa maburungutu ya milioni 10 hadi 40, wengine hata hizo pesa zinawatoa jasho wanapachika vimbao, Pathetic!

Ili uvimbe kwamba una pesa kimjini mjini hasa hapa Dsm basi hakikisha angalau una pesa zinazoweza kuwatisha ama unaendana ama kuwasogelea kwa mbali vijana madoni wenye pesa zao.

Vijana wenye kuweza kumudu milioni 50 ni wengi si haba, hayo maburungutu ya 40 sio levo ya kuvimba.

Angalau uvimbe na dola elf laki 1 sawa na milioni 250 lakini hata ikiwa ni milioni 200 sio mbaya,
1. Cha mtu mavi
2. Bora ndege mmoja mkononi kuliko elfu mtini.

Ringa na chako hata kama buku
 
Raha sana kupiga picha hela
Hata kama ni za ada ya kina Junia 😁
Hata kama ni za rejeshoo
Hata kama huna pa kupost,, bakisha ukumbusho kwenye simu kwamba ulishikaga.

Ilaaaa
Watz na kupangia watu maisha tuna A+

#nisifokewe..
IMG_6829.jpeg
 
Back
Top Bottom