Hawa vijana wanaovimba mtandaoni kwa maburungutu ya milioni 40 ni washamba wa pesa, Ili uvimbe kama don walau uringishie milioni 200

Hawa vijana wanaovimba mtandaoni kwa maburungutu ya milioni 40 ni washamba wa pesa, Ili uvimbe kama don walau uringishie milioni 200

Unakusanya hela zako zinafika milioni 25 unaanza kujirekodi kwamba ni tajirii?

Nimekuja kugundua aina hii ya watu wanatokea vijijini ama mikoani ambako mtu ukiwa na milioni 50 unaonekana doni mtu mzito, sasa wakihamia kwenye jiji wanachukia hawapati ile attention ya vijijini, ndio hapo sasa jogoo la shamba linalazimisha kuwika mjini kwa kujirekodi.

Nashangaa kuona mtu anajisifu ana pesa kisa maburungutu ya milioni 10 hadi 40, wengine hata hizo pesa zinawatoa jasho wanapachika vimbao, Pathetic!

Ili uvimbe kwamba una pesa kimjini mjini hasa hapa Dsm basi hakikisha angalau una pesa zinazoweza kuwatisha ama unaendana ama kuwasogelea kwa mbali vijana madoni wenye pesa zao.

Vijana wenye kuweza kumudu milioni 50 ni wengi si haba, hayo maburungutu ya 40 sio levo ya kuvimba.

Angalau uvimbe na dola elf laki 1 sawa na milioni 250 lakini hata ikiwa ni milioni 200 sio mbaya,
Au atoe ajira kwa watu mia mbili...
 
Raha sana kupiga picha hela
Hata kama ni za ada ya kina Junia [emoji16]
Hata kama ni za rejeshoo
Hata kama huna pa kupost,, bakisha ukumbusho kwenye simu kwamba ulishikaga.

Ilaaaa
Watz na kupangia watu maisha tuna A+

#nisifokewe..
View attachment 2808962
Umenikumbusha kuna siku nilizishika hizi ilinibidi nipige picha kabla ya kuzigeuza madafu
Screenshot_20231109-211825_Photos.jpg
 
Dar es salaam unakuta kijana ana coaster 10 na bado ukaonekana wa kawaida kabisa, ni tofauti na huko vijijini ama mikoani tayari umefika kipimo cha kuitwa tajiri.

Shida inakuja kwa hawa vijana wageni wa jiji wanatokea vijijini ama mikoani walikokuwa wanapata attention ya kuonekana ni matajiri, hawapati tena ile attention waliyoizoea, ndio hapo sasa jogoo la shamba linalazimisha kuwika mjini kwa kujirekodi mitandaoni.

Mtu anajisifu ni don kwa kuonyesha maburungutu ya milioni 30, anahisi bado yupo huko mikoani.

Vijana wenye kuweza kumudu milioni 50 hapa Dsm na hata Mwanza ni wengi si haba, hayo maburungutu ya 40 sio levo ya kuvimba.

Angalau uvimbe na dola laki 1 sawa na milioni 250 lakini hata ikiwa ni milioni 200 sio mbaya, milioni 40 ni za kuvimbia kijijini.
Sawa mkuu, nikizishika sitafanya hivyo maana najua nilipotoka.
 
Wewe kumbe hujui wanaume wa Dar kwenye swala la pesa ndio malimbukeni nambari 1 ,

Nilienda Njombe huko yani kijana unaambiwa ana ghorofa na anamiliki semi 5 yani ukimuona yuko poa sana halafu hata huwezi jua kuwa anapesa hiyo yote ni kama fala hivi
 
Hukunifundisha kutafuta..
Utanifundishaje kutumia
Sheeinzzyyy
Mwaga Hennessy kudadadeki
Leo pesa imekosea njia

Oyaah kwa mabeach boy
Pesa imekosea njia
Oyah kwa mabeach boy
Pesa imejichanganyaa leooo
Leo bill nalipa mie.. pesa imeyatimba

Punguza ushauri watu tuna plan zetu
🎶🎶🎶🎤

Totoo mabantu wakamatwe mshamba_hachekwi
Aisee...
 
Wewe kumbe hujui wanaume wa Dar kwenye swala la pesa ndio malimbukeni nambari 1 ,

Nilienda Njombe huko yani kijana unaambiwa ana ghorofa na anamiliki semi 5 yani ukimuona yuko poa sana halafu hata huwezi jua kuwa anapesa hiyo yote ni kama fala hivi

Kule wanaogopa uchawi. Ukivimba sana wazee hawachelewi kukuchukua msukule
 
Ukivimbia milioni 250 pia wapo watakokwambia hiyo sio ya kuvimbia. Watasema uwe na angalau milioni 700. Ukiwa na hiyo pia kuna watu watakuona hautoshi kuvimba eti tafuta angalau bilioni 2. Kimsingi hata ukiamua kuvimba na 35,000 (elfu thelathini na tano) ni uamuzi wako.

Ni kama tu swala la magari. Unamvimbia asiye na gari kwa kuwa una Raum yako. Mtu mwenye Dualis anaiita baby walker. Halafu anakuja mtu mwenye Discovery anawaona wote hamna magari. Kwamba mna vyombo vya usafiri. Nae wanakuja wenye magari ya pesa nyingi zaidi wanamvimbia. Hata uwe na mafanikio kiasi gani kuna wengi waliokuzidi. Hata uwe masikini wa kiwango gani kuna masikini zaidi yako.

Kwa hiyo nadhani tuache watu wafanye wanayoyapenda kwenye social media. Akaunti yake, bando lake, simu ni yake na pesa ni zake. Akivimba kama hupendezwi scroll down endelea na content nyingine zinazokuvutia.
 
Dar es salaam mji wa kijinga sana , mtu unakuta una coaster 10 na hakuna anayekujua mtaani [emoji3][emoji3]
Jombaa, Thamani ya Coaster 10 mpya kwa kila moja labda weka Tshs. 80M yaani jumla Tshs. 800M ndio thamani ya nyumba za kuishi mitaa mingi ya watu wenye mifuko mipana kama vile Laiboni, Oyster Bay hapo sijaweka hata thamani ya ardhi. Unafikiri ukiishi maeneo kama haya kuna mtu hata anaweza kukufahamu?
 
hizo pesa nafikiri ni za demo, siyo halisi.

zinatengenezwa kwa ajili ya kuigizia, mfano kama zile za kwenye movie au miziki ya Kimarekani
 
Back
Top Bottom