Hawa vijana wanaovimba mtandaoni kwa maburungutu ya milioni 40 ni washamba wa pesa, Ili uvimbe kama don walau uringishie milioni 200

Hawa vijana wanaovimba mtandaoni kwa maburungutu ya milioni 40 ni washamba wa pesa, Ili uvimbe kama don walau uringishie milioni 200

Dar es salaam unakuta kijana ana coaster 10 na bado ukaonekana wa kawaida kabisa, ni tofauti na huko vijijini ama mikoani tayari umefika kipimo cha kuitwa tajiri.

Shida inakuja kwa hawa vijana wageni wa jiji wanatokea vijijini ama mikoani walikokuwa wanapata attention ya kuonekana ni matajiri, hawapati tena ile attention waliyoizoea, ndio hapo sasa jogoo la shamba linalazimisha kuwika mjini kwa kujirekodi mitandaoni.

Mtu anajisifu ni don kwa kuonyesha maburungutu ya milioni 30, anahisi bado yupo huko mikoani.

Vijana wenye kuweza kumudu milioni 50 hapa Dsm na hata Mwanza ni wengi si haba, hayo maburungutu ya 40 sio levo ya kuvimba.

Angalau uvimbe na dola laki 1 sawa na milioni 250 lakini hata ikiwa ni milioni 200 sio mbaya, milioni 40 ni za kuvimbia kijijini.
Wewe unavimba na tumilioni mia ngapi mwana?
 
Kuna kaharufu ka wivu huyo anaesema kuvimba ni mpaka uwe na 200m ukichunguza sana hana hata laki ila anafunsisha watu kuvimba😂😂😂 miache mtu na mali yake pesa zake apate kwa njia yoyote akiamua kuvimba muache ajipost mtandaoni watu wamuone kwan shida iko wapi
 
Kuna sisi ambao hatuna hata million 1 sio cash, bank au assets. Ni haki watuvimbie.
Huna hata ka milioni kamoja benki kweli na upo Jf??..

You must leave this platform ASAP.

Kidding.
 
Jombaa, Thamani ya Coaster 10 mpya kwa kila moja labda weka Tshs. 80M yaani jumla Tshs. 800M ndio thamani ya nyumba za kuishi mitaa mingi ya watu wenye mifuko mipana kama vile Laiboni, Oyster Bay hapo sijaweka hata thamani ya ardhi. Unafikiri ukiishi maeneo kama haya kuna mtu hata anaweza kukufahamu?
Hamna coster ya 80 million
 
Hata vyanzo vya pesa zao havieleweki vimejaa ukakasi, usiumie wala kujilinganisha nao kwa pesa wanazorekodi !!
Hata kama chanzo cha pesa ni halamu as long as anacheza dili zake smart bila kugundulika mbona poa tu.
 
Back
Top Bottom