Hawa Voda ni matapeli au?

Hawa Voda ni matapeli au?

zink

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2021
Posts
1,208
Reaction score
2,352
Habari wakuu wa JF

Katika harakati za kujiunga nikawa napitia menu yao ya vifurushi, na kulingana na vocha nilionunua ya elfu moja a.k.a buku, nikawa nimependa kifurushi ambacho kwa elfu moja kulingana na menu yao ya vifurushi napewa MB 550, dakika 60 na sms 30.

Baada ya kujiunga kifurushi hicho nikaona niangalie salio sasa ile kucheki salio nakuta nimepewa MB 200, dakika 50 na sms 10 badala ya kupewa MB 550 dakika 60 na sms 30 hivi huu si utapeli kabisa tena kwa mtandao mkubwa kama vodacom

Nilichoamua laini yenu navunja, huwa sipendi ujinga mimi narudi zangu TTCL.
 
Wakuu, tususie kuingia internet muda wa mwezi mmoja wapate hasara na serikali ikoswe kodi.
 
Niko zangu Halotel nimerelax,nilivyonunua line kwa 5000 pamoja na kusajili nikapata ofa ya GB 12 mwezi mzima,dk 600 na sms kedekede!

Mwezi ukiisha natupa line,naenda kusajili line nyingine kwa 5000 hiyo napata hiyo mi ofa!Akili mukichwa,jiongezeni ndugu zangu!
 
Hawazidi tiGO, tiGO ni majambazi sugu, kichefuchefu, viazi, wadudu, kimeta, wajinga, zumbukuku, vilaza.

Yani kila nikiwawaza na bando zao za MB 700 kwa 1,500/=Tshs napatwa na hasira sana mamaqeee zao.
Yani sijui kuna shida gani kwenye mitandao mkuu mizinguo tu
 
Hata sijakuelewa mara uwalaumu X uwashukuru mkuu upo km bendera upepo unapoelekea na ww upo
Niimewalaumu sawa ila cha kushangaza wanazidi kujichanganya wananipa adi vifurushi nisivyojiunga sasa siwaelewi mkuu
 
Niko zangu Halotel nimerelax,nilivyonunua line kwa 5000 pamoja na kusajili nikapata ofa ya GB 12 mwezi mzima,dk 600 na sms kedekede!

Mwezi ukiisha natupa line,naenda kusajili line nyingine kwa 5000 hiyo napata hiyo mi ofa!Akili mukichwa,jiongezeni ndugu zangu!
Hhahah hiyo ndo dawa mkuu unapiga kwenye mshono
 
Kuna siku walinifanyia upuuzi unaokaribiana na huu niliwapigia asee wakirudisha dakika zangu na MB
 
Back
Top Bottom