Hawa wa Nitarejea kupelekwa India kwa matibabu,Diamond kutoa zaidi ya mil 50

Hawa wa Nitarejea kupelekwa India kwa matibabu,Diamond kutoa zaidi ya mil 50

umenena vyema, ila kuna jirani yangu mwanaye alikuwa mwizi kupindukia (alikuwa anaitwa mama genai) siku moja mwanaye alipgwa hoi jeshi la polisi likamuokoa, mimi nilimsindikiza mama mzazi kwenda kumuona mwizi aliyepgwa hospitali, nkamwambia mama tunachofanya ni kupingana na jamii kwani ni mwizi ukiingia kwenye 18 zake anaweza kukutoa uhai, majibu aliyonipa mama ndo nataka nkushirikishe wewe, aliniambia hivi,
1. uwe na roho kikristo na usifurahie mtu kupotea katika uovu. tenda wema kama msamaria japo ni ngumu lakini thawabu utazipata mbele.
2. binadamu kwa asili ni mwovu, lakini uchungu wa maumivu kwa mzazi ni sawa sawa na mtoto mwingine hata kama alikuwa kibaka.
niliona anazingua sana. tulivyofika hospitali mama wa mtoto ambaye ni mwizi, alisema kuwa kila siku anamwomba Mungu mtoto wake abadilike lakini sijui ni ile hali ya kukataliwa toka kwa baba yake..
kiufupi. kuwa na roho ya huruma hata kidogo kama angekuwa nduguyo wa damu au mtoto wako usingethubutu kusema haya.
Nimeyasema haya sababu wapo watu walokua wanamshtumu na kumshambulia domo kwamba hamsaidii as if yeye ndo alimtuma akafanye aliyoyafanya.
Nayasema haya sababu nna ndugu kahangaikiwa sana na wanaukoo aache haya mambo. Akikaa anarudia tena, sasa kila mtu kamsusa (kutupa hela kwa mtu mmoja inachosha) lakini wasiojua wamekaa kulaumu eti anaonewa.
 
Wivu unaujua au unaandika andika tu sababu una uwezo wa kuandika. Ukweli utabaki palepale kasaidiwa kama hisani tu haikuwa lazima wala wajibu kama watu walivyokua wanamkaba koo jamaa
Nimekuelewa, nahisi mindset za watu wanaangalia upande hasi wa hili andiko lako.

Kiukweli, jamaa hakuwa na wajibu wa kusema kwamba ni lazima afanye,

Sidhani kama mkataba wao kupiga ile kolabo ulisema jamaaa ataghalamia maisha ya HAWA.

kujitambua tu, haijalishi kwa kuwa mlijenga hit song basi ndio huwe na hatia na maisha yake hivyo.

.ila WELL DONE CHIBU, NDIO UBINADAMU, MUNGU AMSAIDIE HAWA APONE HARAKA
 
Yani wewe ndo umenielewa. Jaribu kutafakari diamond asingetoboa, nani angetoa hiyo hela? Na hii ipo kwa familia pia. Mwisho wa siku wenye watoto zaidi ya mmoja wawafunze watoto wao kupambana ili wasiwe mizigo kwa wenzie na kubaki kusema kaka hanisaidii wakati wazazi wamejitahidi kuwalea kwa usawa ukazembea.
 
Nimeyasema haya sababu wapo watu walokua wanamshtumu na kumshambulia domo kwamba hamsaidii as if yeye ndo alimtuma akafanye aliyoyafanya.
Nayasema haya sababu nna ndugu kahangaikiwa sana na wanaukoo aache haya mambo. Akikaa anarudia tena, sasa kila mtu kamsusa (kutupa hela kwa mtu mmoja inachosha) lakini wasiojua wamekaa kulaumu eti anaonewa.
nimekuelewa sana mkuu.
 
Diamond amefanya Kwa moyo safii tuu...!! Lakini hakustahili kubeba lawamaa kwamba hajamsaidia huyo Dadaa... maana alikuwa anakatazwa Sana na mama akee hakutaka kuachaa kabisa. Leo anaumwa hoii lawama zinaenda kwa diamond kisa alimshirikisha kwenye Nitarejeaa... Ina maana kila alieshirikishwa na diamond akipata shida Diamond Lazima ahusike kumsaidia??? Diamond kafanya kwa moyo ilaa KAMWE HAUKUWA WAJIBU WAKE
 
Hayo ndio machungu ya kutumia vinavyoonywa tunaona twaonewa, Mungu amsaidie arudi salama na atakua kashajifunza
 
Big up sana Mond na hapa ndo bado ntazidi kuwashangaa wanaokufananisha na Kiba! Unamzidi kwa mengi sana kama sio yote! (Povu ruksa)
Kingine kinachonishangaza zaidi bado utakuta kuna msanii mwingine nae anabwia misembe pamoja na mifano yote hii sijui ni nani kawaroga nyie na Industry yenu!!!!?
 
Huo ndio uanaume,sio unakaa kuvua vua machupi 24hrs na kuona ufahari,wakati hata sisi huku kitaa tunayavua sana halafu hamna kinachobadirika.

Mungu akuongezee hela uendelee kusaidia wengine.
 
Back
Top Bottom