Hawa wachezaji bora wa tff, ni umbumbu mwingine.

Zimbe Jr,mchezaji pekee aliyecheza mechi zote za Simba ligi hii dk 90, ndiye mchezaji anayeongoza kwa kucheza dakika nyingi ligi hii kwa kiwango cha juu
huyu Dogo angalau sio kichuya hovyo kabisa
 
sikubaliani na hiyo hoja, timu inaweza kuwa mbovu ila akawemo mchezaji mmoja mzuri ,mfano Abdulrahman Musa wa ruvu shooting, halafu unataka kuniambia kichuya ni bora kuliko Ajibu
 
Hivi ha Tanzania Footaball fungia fungia vigezo wametumia kuchagua hao wachezaj
 
Mwanaume Mashine:

Naanza na Simba
Kichuuuya. Kiboko yao
Mavuuugooo

Naona simba mmelala

Naenda yanga
Tambwe mama kiboko yao
Niyonzima
 
ulianza kuandika kama mtu mwenye akili timamu kumbe ni mwehu kabisa
 
Naona chirwa anasahaulika kwa maksudi huyu jamaa yuko vizuri
 
Kusifia wachezaji kama kichuya.Ndemla.Ajibu.Tsabalala ndio maana ubingwa mnauona kwenye TV...tafuteni watu wa kazi ligi inaboa kila siku sisi Yanga mabingwa
 
Mtazamo wako unataka usamehewe ila tusiwasamehe tff na mitazamo yao eeh? acha double standard mkuu
 
Tukiondoa ushabiki mandazi, hakuna mchezaji mwenye talanta ya juu kabisa VPL kama Shabalala.Nasema hivi kwasababu
1. Shabalala ni mchezaji makini katika nafasi anayocheza,hana rafu za kijinga.
2. Ni beki pekee aliyecheza mechi karibu zote za ligi.
3. Ni mchezaji katika T-stars ambaye ameweza kucheza nafasi hiyo na kuzuia kabisa maadui kupita kwake na kutudhuru.
TUMPAISHE HUYU DOGO atatusaidia maana tukimpa uchezaji bora atauzika nje na kukuuza kipaji chake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…