Hawa wachezaji bora wa tff, ni umbumbu mwingine.

Hawa wachezaji bora wa tff, ni umbumbu mwingine.

Zimbe Jr,mchezaji pekee aliyecheza mechi zote za Simba ligi hii dk 90, ndiye mchezaji anayeongoza kwa kucheza dakika nyingi ligi hii kwa kiwango cha juu
huyu Dogo angalau sio kichuya hovyo kabisa
 
TFF wana vigezo vyao, ukizungumzia wachezaji wa timu zingine nje na Azam, Yanga na Simba
Hao wachezaji ni bora ndio lakini wamefikisha wapi timu zao??
Unataka kumpa uchezaji bora timu yake inashuka daraja

Wache wakapige kura tuone nani atakua bora
Lakini kwa upande wangu hawa watatu wamesaidia sana timu zao "Aishi Manula", " Niyonzima" na "Kichuya"
sikubaliani na hiyo hoja, timu inaweza kuwa mbovu ila akawemo mchezaji mmoja mzuri ,mfano Abdulrahman Musa wa ruvu shooting, halafu unataka kuniambia kichuya ni bora kuliko Ajibu
 
Hivi ha Tanzania Footaball fungia fungia vigezo wametumia kuchagua hao wachezaj
 
Mwanaume Mashine:

Naanza na Simba
Kichuuuya. Kiboko yao
Mavuuugooo

Naona simba mmelala

Naenda yanga
Tambwe mama kiboko yao
Niyonzima
 
ulianza kuandika kama mtu mwenye akili timamu kumbe ni mwehu kabisa
 
Naona chirwa anasahaulika kwa maksudi huyu jamaa yuko vizuri
 
Kusifia wachezaji kama kichuya.Ndemla.Ajibu.Tsabalala ndio maana ubingwa mnauona kwenye TV...tafuteni watu wa kazi ligi inaboa kila siku sisi Yanga mabingwa
 
Salute!
Pamoja na Mimi kuwa mshabiki wa yanga sioni huo uchezaji bora wa msuva ,labda ufungaji. Pia hata huyo kichuya ni hovyo kabisa. Nakwambia hawa wachezaji wawili ni wabahatishaji tu, kubwa ni mbio. Mimi nilitarajia nimuone ndani:
Ibrahim Ajibu(Simba sc)
Haruna Niyonzima(Young Africans)
Yakub Mohammed(azam fc)
Jafari Mohammed(Toto Africans)
Abdulrahman Musa (Ruvu Shooting)
Mbaraka Yusuph(kagera sugar)
Aishi Manula(Azam fc)
Salum Abubakari( Azam fc)
Ikumbukwe huo ni mtazamo wangu ,mnisamehe kwa kweli, ila kwa kuwa majina yameshatoka ni ukweli usiopingika kuwa Haruna Niyonzima ndo bora.
Samahani naomba msnitukane maana kuna watu humu ni waja wa laana.
Mtazamo wako unataka usamehewe ila tusiwasamehe tff na mitazamo yao eeh? acha double standard mkuu
 
Tukiondoa ushabiki mandazi, hakuna mchezaji mwenye talanta ya juu kabisa VPL kama Shabalala.Nasema hivi kwasababu
1. Shabalala ni mchezaji makini katika nafasi anayocheza,hana rafu za kijinga.
2. Ni beki pekee aliyecheza mechi karibu zote za ligi.
3. Ni mchezaji katika T-stars ambaye ameweza kucheza nafasi hiyo na kuzuia kabisa maadui kupita kwake na kutudhuru.
TUMPAISHE HUYU DOGO atatusaidia maana tukimpa uchezaji bora atauzika nje na kukuuza kipaji chake.
 
Back
Top Bottom