Mzee sam
Uteuzi wa mtu katika ubalozi is a funny and tricky way,kisiasa huwa ni njia mojawapo ya kuwaweka mbali trouble makers au kuwapa second life your failed allies.
Sasa ukiangalia uteuzi wa Mapuri nasikitika sijui kwa kweli ana sifa zipi kielimu nashindwa kukupa jibu la ndio au hapana lakini naweza kuchambua utendaji wake:
Huyu bwana ni kada mzuri sana wa chama kiasi ametunga kitabu kuzungumzia mapinduzi ya zanzibar kwa version ya ccm.
Amekuwa katibu mwenezi wa ccm kwa miaka kadhaa.
Alikuwa na blunder baada ya kugombana na waandishi wa habari alipounga mkono kupigwa kwao walipokuwa wakiripoti juu ya nyumba za shirika la mizigo DAHACO.Waandishi waligoma kuandika habari zake akaondolewa hata kwenye kampeni ya Jakaya.
Alikuwa waziri wa mambo ya ndani na sidhani kama alikuwa na mafanikio makubwa, ujambazi ulikithiri sana na idara ya uhamiaji ilikuwa inaboronga mno.
Kwa kufuata impressions sidhani kama alikuwa mtendaji mzuri.
Kwa haya tu nadhani hatujapata mtu safi saaaana kutuwakilisha kule china.
Binafsi ningefurahi kama nafasi ile angepewa Balozi Mlay, ex head wa Tanzania Trade Centre na sasa balozi wa tanzania Ubelgiji, yule mzee ni kichwa kizuri sana na ndio engineer wa sera ya economic diplomacy. Huyu angetufaa sana China ambapo trade opportunities ni kubwa sana na tungeweza kufanya kazi vizuri zaidi na nchi hii lakini JK ameamua kuendeleza mahusiano yetu na china katika medani ya siasa zaidi kuliko biashara manake mapuri is good for politicking lakini kibiashara na diplomasia ya uchumi tumehola.
Naam kuna mmoja mwenzetu amechangia kuhusu swali la msingi ni kama china inaweza kutukomboa au la, kimsingi hawawezi mkombozi wa kweli ni sisi wenyewe lakini tunaweza kujifunza mengi toka china katika kujiendeleza.