Hawa wadada wenye majina makubwa wanatoa wapi pesa za matanuzi?

Hawa wadada wenye majina makubwa wanatoa wapi pesa za matanuzi?

Kilemakyaaro

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2016
Posts
5,051
Reaction score
5,104
Nikimuona Diamond na kina Kiba na wanamuziki wengine wakila bata najua ni mziki wao unawalipa. Ila kuna hawa watu maarufu huko Instagram kama kidada fulani Tunda na wengine, picha zao zimekaa kibatabataaa lakini niulize huwa wanafanya kazi gani maana hata kama ni kuimba kama hata wamewahi jaribu bado hawana majina makubwa, hawaonyeshi kumiliki labda hata mabiashara.

Hebu jamani kama wapo humu watuambie kazi zao maana hata kulalama njaa kama wengine wanaolialia hawasikiki.

Tafakuri tu japo ni maisha ya watu hayanihusu
 
Kiuno mkuu!
 
Ni moja wapo wa madada ambao "K" zao zinatafutwa mno Dsm, na kwa sababu hiyo wale wenye pesa tu ndio huzipata tena kwa kuwagharamia hizo unazoziita BATA!!

Japo kiuhalisia ni maskini tu ambao hata wewe hawakufikii kiuchumi!!
 
Sasa nimepata picha japo wapo waliokejeli lkn nimejifunza, huku mtaani kuna wadada wanapambana sana na maisha kusema kweli, kwa mfano wapo wale wadada makonda wa daladala huwa wananifanya nickate tamaa haswa kipindi kile nikiwa cna kazi,nlimaliza chuo kikuu na nikawa machinga kariakoo,nikanyoa saluni lkn kusema kweli moja ya watu waliokua wananifanya nikomae ni kumuona binti yupo mlongoni mwa daladala alaf mimi nishindwe kukomaa na jiji nirejee kijijini ambako hamna ramani kwa kitambo hicho
 
Wanafumuliwa Marinda kila kukicha,

Wengine ndio wabeba Unga maarufu.
 
Wala usije ukatamani kuvaa viatu vyao, hutoviweza...wewe baki tu kuwaangalia huko huko insta.
 
Tunda babake askar tu alikuwa anaitwa sabasita wakati anafanya kaz Moro ..watoto wanatumia viungo vyao vizuri haooo hahahaaa
haaaa!!!!! Hivi kumbe huyu Tunda ndo yule mtoto wa Sabasita.....!!!!! Ama kweli maisha yanakwenda kasi....mimecheza nae kibaba jmn daah
 
Back
Top Bottom