Hawa wakimbiza mwenge kitaifa huwa wana sifa(vigezo) gani?

Hawa wakimbiza mwenge kitaifa huwa wana sifa(vigezo) gani?

Dogo G

JF-Expert Member
Joined
Jul 6, 2018
Posts
1,052
Reaction score
440
Habari wakuu,huwa najiuliza na huwa sipati majibu ila leo nimeona nivunje ukimya.

Hawa wakimbiza mwenge kitaifa huwa wana sifa(vigezo) gani?,nikiimaanisha je ili mtu yeyote ateuliwe kukimbiza mwenge wa uhuru kitaifa awe na sifa zipi?,je,wanapatikana majeshini i.e JWTZ,POLISI au MAGEREZA ama wanatafuta watu wenye taaluma kubwa?

Elimu yenu wakuu,
FB_IMG_15312523426668591.jpg
 
Kwanza kabisa uwe na kadi ya ccm.

Pili uijue vyema ILANI ya chama dola.
Mh mkuu ndio wanavyopatikana hivyo? Basi hata mimi niliyeishia la tatu B ningeteuliwa maana mwaka wa kumi huu nna kadi ya chama
 
Mkuu nifafanulie kidgo maana sina bible nyumbani
Nitafanya kwa heshima Na taadhima kwako.
Isaya : Mlango 50

11 Tazama, ninyi nyote mwashao moto, mjifungiao hiyo mienge; endeni ninyi katika mwali wa moto wenu, na katikati ya mienge mliyoiwasha. Mtayapata haya kwa mkono wangu; mtalala kwa huzuni.
 
1.Lazima huwe umekunywa juisi ya bendera ya chama
2.Hakikisha kuwa kuanzia mlangoni kwako kuna pazia la kijani,mezani na madirishani vitambaa vya kijani.
3.Lalia mashuka ya kijani na familia yako nzima.
Jaribu uone maajabu!😀😀😀😀😀😵
 
Habari za Vijiweni zilikuwa zinadai baada ya kukimbiza mwenge kiongozi wa mbio hizo ana Rest in Peace.
 
Nitafanya kwa heshima Na taadhima kwako.
Isaya : Mlango 50

11 Tazama, ninyi nyote mwashao moto, mjifungiao hiyo mienge; endeni ninyi katika mwali wa moto wenu, na katikati ya mienge mliyoiwasha. Mtayapata haya kwa mkono wangu; mtalala kwa huzuni.
Sasa uhusiano na topic uko wap apo mkuu bujibuji
 
1.Lazima huwe umekunywa juisi ya bendera ya chama
2.Hakikisha kuwa kuanzia mlangoni kwako kuna pazia la kijani,mezani na madirishani vitambaa vya kijani.
3.Lalia mashuka ya kijani na familia yako nzima.
Jaribu uone maajabu!😀😀😀😀😀😵
Umetisha mkuu
 
Back
Top Bottom