Hawa waliotuletea network marketing wanatumalizia vijana wetu ari yakutafta pesa

Mkuu nilishawahi fanya kazi kwenye kampuni moja hivi ya kusambaza vyombo,yaani nilifanya kazi mwezi mzima nakuja kuambia kwenye akaunti yangu nina 2300,mbona niliondoka na vyombo vyenyewe
πŸ˜‚πŸ˜‚Umenimaliza kwa cheko
 
Qnet walimteka mdogo wangu na maneno mazuri anakuja na habari za million tano saa uzuri kuna nyuzi nilisoma humu nikamzaba makofi mbele ya mama ake akili ipo sawa
safi sana. Uliplay smart! Kuna mshkaji nilimnusuru asimchinje GF wake, Kisa GF kapeleka 5m Qnet! Alitaka kumkata shingo! Heri yako ulimchapa kelbu huyo dogo!
 
huwa wanatoa ahadi kubwa mno za mafanikio,kiuhalisia hizi ni biashara kama biashara zingine, kuna kupata au kukosa, ndio maana kuna wanaofanikiwa na wasiofanikiwa. Mimi niliifanya miaka mitatu nikaachana nayo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…