Kiongozi sahihi wa kuipeleka Tanzania mbele atatoka upinzani na si ndani ya ccm! Maana huyu ni sawa na mchezaji wa akiba aliyetoka nje ya uwanja kwani anakuwa ameshayaona mapungufu yote! Hata hapa majuzi Membe amekiri ukiwa ndani ya ccm huwezi kuyaona mapungufu yake wala ya serikali yake!
Zaidi ya yote hata ukija kuyaona hutaweza kuyafanyia kazi sabab kwa namna moja au nyingine utakuta mfumo huohuo ndio uliokuzaa na kukupa madaraka unayokuwa nayo!
Mfano JK alishindwa kushughulikia wizi wa EPA ambao ulifanyika awamu ya 3 coz ndo ulowezesha akaingia ikulu, JPM na makeke yake yote ya kufungua hadi mahakama za mafisadi, lakini alishindwa kuwagusa waliochota mabilioni ya nssf, sabab zinajulikana!
Hivyo kiongozi wa kutufaa ni wa kutoka upande wa pili tu!