MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Wakuu haihitaji research yoyote ya kisayansi kujua umuhimu wa kula. Pia haihitaji research kujua kuwa watanzania wengi hawapati chakula cha kutosha achilia mbali balanced diet. Yaani hata ugali maharage wa kushiba ni changamoto. Mimi nimeishi maeneo ya uswahilini Dsm nikaona mwenyewe jinsi watu wanashinda na njaa... kimsingi wanakula hawashibi. Vidonda vya tumbo ni sehemu ya maisha yao. Tatizo la lishe duni ni kubwa mno.
Serikali izuie hawa wataalamu feki wanaoeneza taharuki mitandaoni kwa kutamka karibu kila chakula kina madhara. Ugali, matunda, asali, chapati, wali, viazi, hata nyama choma zimetajwa kuwa hazifai. Wanaharakati wengine wameenda mbali zaidi kuwa kutaka watu wapuuze yote waliyofundishwa shuleni kuhusu vyakula. Wanadai tulidanganywa. Kuna mmoja anasema hakuna haja ya breakfast.
Hawa watu wasipodhibitiwa watazidi kuleta taharuki na wananchi kuwa dhaifu kwa kutokula vizuri. Tutakuwa taifa goigoi. Wizara ya afya itoe tamko kuhusu wenye uhalali wa kuongelea afya na mambo ya vyakula na sio kila mtu ajiamulie kisa ni fitness trainer.