Hawa wanajiita wanamuziki lakini mimi nasema ni wahuni na wababaishaji

Nsimbi

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2014
Posts
1,091
Reaction score
1,203
Wanajiita wanamuziki lakini mimi nasema ni wahuni na wababaishaji ambao wameivamia fani kwa mtindo wa zima moto.

Baadhi ya wanamuziki wanaojiita ni wa kizazi kipya ni janga kwa taifa kwa kuwa wanaiharibu jamii kwa nyimbo zao za ovyoovyo.

Wengi ni wachafuzi wakubwa wa lugha na ni tishio kwa malezi ya watoto wadogo. Ni rahisi kwa mtoto kuiga kuvaa mavazi ya ajabu kwa vile amemuona mwanamziki maarufu kwa luninga.
Mtoto wa kiume akimuona mwanamziki wa kiume kavaa gauni au kusuka nywele ni rahisi kudhani kuwa hiyo ni sawa.
Mtu kama Diamond Platinum ni mfano mbaya kabisa kwa watoto. Mambo yake mengi ya ovyo yanaigwa na watoto na ni vigumu kuwakataza.
Hana nyimbo zozote za maana zaidi ya bahati tu inayombeba. Zile tetesi za ndumbanangai labda si uongo kwani hana nyimbo zenye viwango. Amewapumbaza watu kupenda nyimbo zake zilizojaa utumbo wa taulo?
Huyu kijana sasa fedha zinamlevya ameanza nyodo.

Hata Ali Kiba hana la maana. Mashabiki wanawavimbisha tu vichwa vijana hawa ni hivyo kuwafanya wadhani wanaimba nyimbo nzuri kumbe sivyo.
Watu kama Hamorapa ndio wanamuziki wa ovyo ninaoongelea. Sijui hata anaimba nini. Baadhi ya wananchi wanapenda nyimbo mbaya. Dodojanja anajitahidi kiasi ingawa hana jipya. Sister P anajiita mkongwe lakini nahisi analazimisha tu. Hana kipaji.
Kibonge mwepesi anaweza kuwa na kipaji sema bongofleva imekorogwa sana siku hizi.

Yule Snura naye analazimisha tu. Hana kipaji cha muziki kabisa. Chura atachuja sana kwani nyimbo zake hazina ujumbe wala vina.
Barnaba ni mbabaishaji mkubwa. Analazimisha kazi asiyoiweza. Sioni nyimbo zozote za maana zaidi ya kuvaa kike na hivyo kupotosha watoto wetu.
Shishibabe anabananga sema ana bahati ya kupendwa. Yeye anadhani watu wanapenda nyimbo zake kumbe wanamuonea huruma!
Maua Sama naye kituko jumlisha rafiki yake Gigimoney. Hawa wanafinyanga maadili ya taifa na kuwa sumu kwa makuzi ya watoto.

Vanessa anaupenda musiki lakini musiki haumpendi yeye. Ulaghai tu unambeba lakini nyimbo zake hazina mashiko.

Mwasiti anajikongoja sema amezongwa na msitu wa wanamuziki vimeo.
Utitiri wa wanamuziki ganga njaa unafanya wenye vipaji kubaniwa.

Wengi wamevamia fani ya musiki kwa kukwepa kazi ngumu lakini za staha kama kilimo, useremala, uvuvi, uchimbaji madini nk. Wengine walikwepa ugumu wa shule.

Mtu yeyote anaweza kuimba lakini si kila mtu anaweza kuwa mwanamziki. Lazima uwe na kipaji. Huwezi kufoji kipaji.
Jamii iache kuwashobokea wana bongofleva wahuni.
 
Ukitaka waimbe kama unavyotaka mimi na wewe wasingejulikana ila upuuzi wanaofanya watu ndo wanata angali watu kama nikki mbish,i songa, nash mc, wachache wanawafahamu wamebaki katika misingi ya hip hop yenyewe ila hawatambuliki ila mtu kama nay wa mitego, dogo janja ndoo waimba hip hop wanaofahamika so siku izi wasanii wanafanya nini mashabiki wanataka
 
MKUU TUANZE NA WEWE,UNA KIPAJI GANI KWA MFANO??!!!
Na kama hao hawana kipaji toa japo wimbo mmoja ujulikane nchi nzima kisha uje uwatoe akili hao jamaa
Mi nilikuwa naponda sana wasanii kuna siku nikaenda studio kwa rafiki yangu.Kufika si akaniambia niingie vocal room.Akaweka biti akaniambia jaribu kuingiza maneno.Nilibaki najiuma uma tu
HESHIMU KAZI ZA WATU MKUU
 
Acha kusikiliza kazi zao kesi itakuwa imeisha ila huwezi kulazimisha unachochukia wewe dunia nzima ichukie
 
Kibongobongo mtu ukiona mbali na ukitoa mawazo yenye ukweli ndani yake katika kitu kilicho wazi utasutwaaàa utapingwaaa utasulubishwaa utaambiwa vitu ambavyo vitakutoa kwenye right track!!!! utaletewa pumba ambazo ukizitia maanani utajikuta umepumbazika

Much respect mtoa mada
 
Muziki ni aina ya sanaa inayotumia sauti mbalimbali: za kibinadamu na za ala za muziki, ama kwa pamoja au kila moja
pekee.

Asili ya neno lipo katika lugha ya Kigiriki ambamo huitwa μουσική (mousikee).

Baadhi ya sifa za muziki ni
-uzito wa sauti (pitch)
-wizani au mahadhi (rhythm).

Aina ya muziki inayopatikana kote duniani ni nyimbo ambazo ni maneno yanayotolewa kwa sauti na mahadhi fulani mara nyingi
pamoja na ala za muziki.

Kwa wanaorekodi sauti, wao huenda
kwa studio kurekodi na
huchukuliwa kwa kinasasauti kilicho ambatanishwa na tarakilishi na kudhibitiwa na kompresa..
 
mtoa mada hv ile nyimbo yako yenye maadili inaitwaje ?
 
Mimi naongezea waimba singeri wote wanachafua sanaa. siwapendi Kama wamo humu wanisamehe kwa maneno yangu makali
 
naomba tu niheshimu mtazamo wako kwakweli maana sijui hata umeongea matapishi gani but ndo hvyo tena hatushei ubongo
 
Mlipuko wa ugonjwa wa waimbaji wa hovyo unawaharibia njia wanabongofleva wenye akili, mahiri na vichwa kama 20 per cent.
Utitiri wa wanamuziki vimeo unawazibia vichwa kama Mh Temba, Mandojo, Inspector Haruon, Chege, GK, Iranga, Zongo, Ferouz, yule "mzee wa ugali", jamaa wa t.shirt na jeans nk.
Kuzuka kwa virusi kwenye anga la bongofleva kumewapoza vichwa vingine kama mama wa sugua gaga na yule wa summer jam!
 
Hamia huku zilipendwa nyimbo za jazz band
Hutojuta!!
Achana na hao wababaishaji na mashalawadu
 
Muziki biashara, huku bongo mwenye kipaji hatambi ila wenye njaa ya vipaji ndiyo wanaobamba mtaani na majukwaani.
 
UKWELI KAMA WOTE.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…