Wanajiita wanamuziki lakini mimi nasema ni wahuni na wababaishaji ambao wameivamia fani kwa mtindo wa zima moto.
Baadhi ya wanamuziki wanaojiita ni wa kizazi kipya ni janga kwa taifa kwa kuwa wanaiharibu jamii kwa nyimbo zao za ovyoovyo.
Wengi ni wachafuzi wakubwa wa lugha na ni tishio kwa malezi ya watoto wadogo. Ni rahisi kwa mtoto kuiga kuvaa mavazi ya ajabu kwa vile amemuona mwanamziki maarufu kwa luninga.
Mtoto wa kiume akimuona mwanamziki wa kiume kavaa gauni au kusuka nywele ni rahisi kudhani kuwa hiyo ni sawa.
Mtu kama Diamond Platinum ni mfano mbaya kabisa kwa watoto. Mambo yake mengi ya ovyo yanaigwa na watoto na ni vigumu kuwakataza.
Hana nyimbo zozote za maana zaidi ya bahati tu inayombeba. Zile tetesi za ndumbanangai labda si uongo kwani hana nyimbo zenye viwango. Amewapumbaza watu kupenda nyimbo zake zilizojaa utumbo wa taulo?
Huyu kijana sasa fedha zinamlevya ameanza nyodo.
Hata Ali Kiba hana la maana. Mashabiki wanawavimbisha tu vichwa vijana hawa ni hivyo kuwafanya wadhani wanaimba nyimbo nzuri kumbe sivyo.
Watu kama Hamorapa ndio wanamuziki wa ovyo ninaoongelea. Sijui hata anaimba nini. Baadhi ya wananchi wanapenda nyimbo mbaya. Dodojanja anajitahidi kiasi ingawa hana jipya. Sister P anajiita mkongwe lakini nahisi analazimisha tu. Hana kipaji.
Kibonge mwepesi anaweza kuwa na kipaji sema bongofleva imekorogwa sana siku hizi.
Yule Snura naye analazimisha tu. Hana kipaji cha muziki kabisa. Chura atachuja sana kwani nyimbo zake hazina ujumbe wala vina.
Barnaba ni mbabaishaji mkubwa. Analazimisha kazi asiyoiweza. Sioni nyimbo zozote za maana zaidi ya kuvaa kike na hivyo kupotosha watoto wetu.
Shishibabe anabananga sema ana bahati ya kupendwa. Yeye anadhani watu wanapenda nyimbo zake kumbe wanamuonea huruma!
Maua Sama naye kituko jumlisha rafiki yake Gigimoney. Hawa wanafinyanga maadili ya taifa na kuwa sumu kwa makuzi ya watoto.
Vanessa anaupenda musiki lakini musiki haumpendi yeye. Ulaghai tu unambeba lakini nyimbo zake hazina mashiko.
Mwasiti anajikongoja sema amezongwa na msitu wa wanamuziki vimeo.
Utitiri wa wanamuziki ganga njaa unafanya wenye vipaji kubaniwa.
Wengi wamevamia fani ya musiki kwa kukwepa kazi ngumu lakini za staha kama kilimo, useremala, uvuvi, uchimbaji madini nk. Wengine walikwepa ugumu wa shule.
Mtu yeyote anaweza kuimba lakini si kila mtu anaweza kuwa mwanamziki. Lazima uwe na kipaji. Huwezi kufoji kipaji.
Jamii iache kuwashobokea wana bongofleva wahuni.