Hawa wanamichezo wa enzi hizo wako wapi..?

Hawa wanamichezo wa enzi hizo wako wapi..?

PRINCEd

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2015
Posts
860
Reaction score
620
Jana katika pita zangu nikakutana na Kipande cha Gazeti katika nyumba ya babu yake na rafiki yangu, kikiwa kimebandikwa ukutani kikiwa na majina ya wachezaji wazamani....

Nikataman kujua wako wapi na wanafanya nini kwa Sasa

1. Jera Mtagwa
2. Ibra Washokela
3. George Masatu Kisiki
4. Wastari Baribari
5. Manara wote wawili
6. Fumo Felician
7. Quresh Ufunguo
8. Mwanamtwa Kiwelu
9. Thobias Gaga (gagarhino)
10. Nteze John Rungu
11. Edibily Jonas Lunyamila
12. Saidi maulidi SMG
13. Makumbi Juma
14. Abeid Mziba
 
Jana katika pita zangu nikakutana na Kipande cha Gazeti katika nyumba ya babu yake na rafiki yangu, kikiwa kimebandikwa ukutani kikiwa na majina ya wachezaji wazamani....

Nikataman kujua wako wapi na wanafanya nini kwa Sasa

1. Jera Mtagwa
2. Ibra Washokela
3. George Masatu Kisiki
4. Wastari Baribari
5. Manara wote wawili
6. Fumo Felician
7. Quresh Ufunguo
8. Mwanamtwa Kiwelu
9. Thobias Gaga (gagarhino)
10. Nteze John Rungu
11. Edibily Jonas Lunyamila
12. Saidi maulidi SMG
13. Makumbi Juma
14. Abeid Mziba
Baada ya kuitumikia jamii kupitia sanaa na muda wao kwisha yalianza maisha ya kupungua umaarufu au umaarufu kwisha kabisa na sasa ni raia wa kawaida tu
..khamis thobias gaga alikwisha tangulia mbele ya haq.kuhusu Manara wapo Sunday kasimu na kitwana watu wazima hao. Huyu ibra sikumbuki ila kama ungesema James washokera alikuwa mkoba wa ushirika moshi na pia pamba ya mwanza.
 
# 13 alishafariki
# 11 huyo yuko mbezi ya kimara huko
#10 aliendaga marekani kitambo sjui kama alirudi

Ova
 
13 yupo leaders club kila jumapili akifanya mazoez na akna idd azan,maisha anayoishi sio ya kuish homa ya jiji niliemjua mimi,umri umemuacha sana ila bdo anajitahid kunyönga baiskel wakat idd azan ambae miaka ile alikuw dreva teksi wake pale Fire sasa anatembelea Jeep!,maisha haya......!
 
Hamis Gaga nakumbuka alipatwaga sekeseke la ujambazi

Ova
Sikumbuki ila alikuwa mtu wa kunywesha sana na hana kitu mpaka kukawa na story watu wanaharibu. Kuhusu watu wa kazi pana beki mmoja wa kati wa simba pana siku kaharibu mchana kweupe tazara pale kinomanoma mwengine ni Michael poul nylon nae alikuwa kimtindo na michezo hiyo hasa ya magari. Jujuman pia wanadai alikuwa mtu wa ngoma (mkwaju )baada ya mambo ya mpira kuisha.
 
Jela Mtwaga bado yupo hai japo ana KIHARUSI... Juzi tu Waziri Mwakyembe alimtembelea kwake Daaah anakaa mabondeni huko Manzese. Akaahidi kumhamishia sehemu rafiki ili aweze kufanya Mazoezi...
 
Hivi George Lucas Gaza yupo wapi sasa hivi?

Jamaa kawa matawi sana sasa hivi huko America hadi rangi kabadilika kabisa ..
20190902_155539.jpg
 
Back
Top Bottom