GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
Kuna Mmoja kapanda Dala Dala nililopanda Jana Usiku la Buguruni - Mwenge aliniachi Maswali mengi sana.
Kwanza ana Afya nzuri ambayo hata GENTAMYCINE ninayeombwa Msaada sina.
Pili kuna muda akasema kuwa tayari ana Shilingi Milioni Saba na anataka tumchangie Shilingi Mia Tano, Elfu Moja zetu na tulizojaaliwa nazo ili akatibiwe nchini Uingereza.
Tatu na hapa ndipo si tu alinichanganya bali alinikera pia alikuwa anajielezea kwa ufasaha huku akitaja Ugonjwa wake Kisayansi / Kitabibu kabisa na Kujiamini Kwingi mpaka pale macho yangu Makali na yanayotisha yalipogongana nae akaomba Kondakta amshushe Kituo cha mbele huku akiiacha Hela aliyokuwa akipewa na Abiria wa Siti ya Nyuma.
Kwa wale wapanda Bayankata (Daladala) Wenzangu wa hiyo Route ya Buguruni hadi Ubungo River Side huenda huyu Mbaba mtakuwa mnamjua.
Kimwonekano na kwa Afya yake Njema nahisi ni Mhaya au Mnyakyusa na ana POP la Shingoni na ni Hodari wa Kutia Huruma, Kujionyesha anaumwa kweli kweli.
Akiona hakuna anayehangaika nae Kumpa Msaada anaanza Kuwahubirieni huku akiamka Kitini na kutembelea Siti zenu Abiria kwa mwendo wa Mgonjwa Mgonjwa ( wa Kiunyonge na Kiutaratibu ) ila akiona kuna Abiria anataka kumpa Pesa anabadili mwendo na kutembea vizuri na kwa Kasi ya 5G kabisa.
Leo GENTAMYCINE kwa Makusudi napita tena njia hiyo hiyo nikitoka Kushuhudia Marumo Gallants FC wakimfunga Mtu na nikikutana nae simkawizi Namchana makavu kwani kwa nilivyomsoma kwa Saikolojia yangu Kali ya Kuzaliwa nayo, ya Kimaono na ya Kusomea nimegundua kuwa Anatuokota / Anatudanganya tu.
ANGALIZO
Kwa Wewe KISOKOLOKWINYO ( MUWASHWAJI MUWASHWAJI ) na Mpumbavu ( Damn Fool ) unayejijua humpendi GENTAMYCINE na Mada zake / Uwasilishaji wake hapa JamiiForums tafadhali TUSICHOSHANE na acha kabisa Kusoma na hata Kuchangia bali Watafute Members wengine unaowaona ni Bora Kwako na Unawakubali kuliko Mimi.
Nimemaliza