kanene, hilo tatizo siyo lako peke yako kaka. Wengi sana wamekuwa na wakati mgumu kwenye ndoa kutokana na kutopata watoto. Lakini umenitisha uliponambia wife anazalisha hormone za kiume badala ya kike? Aliyewaambia haya ni daktari ambaye yupo serious kweli? Achana na hayo maneno ya daktari. Kwani mke wako ni mnene sana? Sometimes too much fat in the body, huwa inaweza ikaharibu mfumo wa kawaida wa uzalishaji wa hormones mwilini.
Lakini nakushauri ufanye majaribio yafuatayo:
1. Hesabu kwa umakini mkubwa kabisa siku za mke wako ili ujue mzunguko wake upoje?
2. Kama atakuwa ana mzunguko wa siku 28, basi jipe mtihani mgumu, tangu kuanza kwa bleed usile mzigo kabisa hadi kufikia siku ya 13 ndo ule. (Hii itakusaidia hasa kama tatizo lipo upande wako kwa maana ya kwamba unazalisha mbegu ambazo hazijakomaa. Naamini for two weeks zitakuwa zimeshakomaa). Angalia pia position mnayotumia kulingana na umbo la mkeo, na pia usiwe na haraka ya kuchomoa mara baada ya kumaliza. Mara nyingi kifo cha mende kwa kukunja miguu kuelekea mabegani yaweza kuwa ni style nzuri zaidi.
3. wakati huu wote mke wako pamoja na wewe mwenyewe jitahidini kula kwa wingi vyakula vifuatavyo: Soya kwa wingi (zinapatikana sokoni hizi) mboga majani kwa wingi sana, mazao ya mikunde - kwa maana ya karanga na vitu kama hivyo, na matunda kwa sana.
4. mtahitaji pia vitamin E ya kutosha, hii mnaweza kuipata kutoka kwenye vyakula hivi: Mayai, parachichi, korosho, karanga, kunde, na mboga za majani. Hizi mboga msipende sana kula zilizopikwa na kuungwa, zichemsheni kidogo tu na kuzila - hakikisha haibadiliki rangi. Si lazima ule wakati wa msosi, unaweza kula kama dozi.
5. Bila shaka unazifahamu tetele (mbegu za maboga), humu kuna zinc ya kutosha sana, na ni mhimu sana kwa mwanamke kwa ajili ya kurutubisha yai. Kama mnaweza kuzipata basi mnaweza kuamua kufanya utaratibu wa kuunga hizo kwenye mboga zenu.
6. Kama kuna mmojawenu anatumia kilevi au sigara ni vema aache katika kipindi hiki cha kutafuta mtoto.
Inawezekana hii njia isifanye kazi mwezi wa kwanza tu wa huu mpango lakini ikafanya kazi mwezi unaofuata. Lakini kama mkeo ni mnene sana basi anza kwanza process za kushughulikia kupunguza unene wake. Maana hilo ni tatizo sana kwenye kushika mimba kuna tafiti kabisa zinazoonyesha kwamba asilimia kubwa ya wanawake wanene wana shida katika kushika mimba.
Nitashukuru kama utanipa feedback baada ya kufanikiwa.
Best wishes!