Hawa wanaweza kupata watoto?

Hawa wanaweza kupata watoto?

kanene

Member
Joined
Jan 25, 2012
Posts
55
Reaction score
6
Habari zenu wana jf. Samahani ndugu zangu naomba kuuliza kwamba hivi mwanaume na mwanamke wakiwa wana blood group moja wanaweza kupata mtoto? yaani kwa mfano mwanaume ana group O positive,na mwanamke ana group O positive. Hawa wawili wakioana wanaweza kupata mtoto? na kama hawawezi ni kwanini,na ili wapate mtoto nini kifanyike? Naomba ufafanuzi ndugu zangu
 
Blood group haina shida kwenye suala zima la upatikanaji wa mtoto. Chenye shida ni rhesus factors. Na mara nyingi huwa inakuwa shida kama mwanamke atakuwa na rhesus factor -ve, kwa maana ya blood group O negative. Lakini kwa kuwa wako ni positive basi hakuna shida kabisa. mtapata mtoto mwenye afya zote. Sema tu kwa kuwa blood group yenu ipo controlled na recessive gene, mtoto wenu pia atakuwa na blood group O positive. Otherwise uwe na amani kabisa.
 
asante sana mkuu ila naomba unieleweshe kidogo hizo sehemu zenye blue...samahani kwa usumbufu
 
Hizo rhesus factors ni blood protein ambazo ndizo zinazofanya hiyo blood group yako iitwe O positive au negative. Kwa hiyo wakisema ni positive ina maana kuna hizo protein zinazoitwa rhesus factor na ikiwa negative ina maana hizo rhesus factor hazimo. Kama itatokea mama akawa hana hizi protein halafu amepata mimba kutoka kwa mwanaume mwenye nazo, huwa zinatabia ya kufanya kitu kinaitwa blood clotting ambayo ni kama kuganda kwa damu ya mtoto na hivyo mimba iliyotungwa inaweza kuharibika tangu ikiwa tumboni au mtoto akafariki mara tu baada ya kuzaliwa.

Ila hiyo recessive gene nafikiri itakuwa kazi ngumu sana kukueleza, kwa maana inahusika na mambo ya crossbreeding kwenye mambo ya genetics. Sasa hilo litakuwa ni soma refu. Cha msingi elewa kwamba wewe na mchumba wako mna mbegu zinazofanana kwa hiyo mtapata mtoto mwenye blood group kama ya kwenu. Ina maana kama angekuwa mmojawenu amechanganya labda ana AO, basi mngeweza kupata mtoto mwenye blood group A. Lakini sioni umhimu wa wewe kujua sana habari za genetic kwa kuwa hazina impact yoyote kwenye kuzaa kwenu na kukua kwa mtoto wenu. Just go ahead na mpango wenu wa kuzaa.
 
mkuu asante sana ila kwa kifupi labda nikuweke wazi kwamba nina miaka 6 tangu niwe na huyu mchumba wangu cha ajabu tumehangaika sana bila mafanikio. nimetembelea hospital nyingi na mpaka sasa hakuna tumaini kwani vipimo vinaonyesha yeye hana tatizo na mimi sina tatizo. kuna wakati tuliambiwa mwili wake unazalisha hormon za testestrogen badala ya kuzalisha oestrogen...na kuna wakati siku za hedhi zinapotea hata miezi mitatu
 
Poleni sana mkuu, msikate tamaa, kwa Mungu hakuna kubwa, endeleeni kuishi kwa amani ila msiwe na tention saana
wakati wa tendo la ndoa, mnatakiwa mrelax kana kwamba mko kwenye uzazi wa mpango badala ya kukazania kupiga goli !!
 
Asante sana mkuu.... asante kwa ushauri wako
 
mkuu asante sana ila kwa kifupi labda nikuweke wazi kwamba nina miaka 6 tangu niwe na huyu mchumba wangu cha ajabu tumehangaika sana bila mafanikio. nimetembelea hospital nyingi na mpaka sasa hakuna tumaini kwani vipimo vinaonyesha yeye hana tatizo na mimi sina tatizo. kuna wakati tuliambiwa mwili wake unazalisha hormon za testestrogen badala ya kuzalisha oestrogen...na kuna wakati siku za hedhi zinapotea hata miezi mitatu

kanene
, hilo tatizo siyo lako peke yako kaka. Wengi sana wamekuwa na wakati mgumu kwenye ndoa kutokana na kutopata watoto. Lakini umenitisha uliponambia wife anazalisha hormone za kiume badala ya kike? Aliyewaambia haya ni daktari ambaye yupo serious kweli? Achana na hayo maneno ya daktari. Kwani mke wako ni mnene sana? Sometimes too much fat in the body, huwa inaweza ikaharibu mfumo wa kawaida wa uzalishaji wa hormones mwilini.

Lakini nakushauri ufanye majaribio yafuatayo:

1. Hesabu kwa umakini mkubwa kabisa siku za mke wako ili ujue mzunguko wake upoje?

2. Kama atakuwa ana mzunguko wa siku 28, basi jipe mtihani mgumu, tangu kuanza kwa bleed usile mzigo kabisa hadi kufikia siku ya 13 ndo ule. (Hii itakusaidia hasa kama tatizo lipo upande wako kwa maana ya kwamba unazalisha mbegu ambazo hazijakomaa. Naamini for two weeks zitakuwa zimeshakomaa). Angalia pia position mnayotumia kulingana na umbo la mkeo, na pia usiwe na haraka ya kuchomoa mara baada ya kumaliza. Mara nyingi kifo cha mende kwa kukunja miguu kuelekea mabegani yaweza kuwa ni style nzuri zaidi.

3. wakati huu wote mke wako pamoja na wewe mwenyewe jitahidini kula kwa wingi vyakula vifuatavyo: Soya kwa wingi (zinapatikana sokoni hizi) mboga majani kwa wingi sana, mazao ya mikunde - kwa maana ya karanga na vitu kama hivyo, na matunda kwa sana.

4. mtahitaji pia vitamin E ya kutosha, hii mnaweza kuipata kutoka kwenye vyakula hivi: Mayai, parachichi, korosho, karanga, kunde, na mboga za majani. Hizi mboga msipende sana kula zilizopikwa na kuungwa, zichemsheni kidogo tu na kuzila - hakikisha haibadiliki rangi. Si lazima ule wakati wa msosi, unaweza kula kama dozi.

5. Bila shaka unazifahamu tetele (mbegu za maboga), humu kuna zinc ya kutosha sana, na ni mhimu sana kwa mwanamke kwa ajili ya kurutubisha yai. Kama mnaweza kuzipata basi mnaweza kuamua kufanya utaratibu wa kuunga hizo kwenye mboga zenu.

6. Kama kuna mmojawenu anatumia kilevi au sigara ni vema aache katika kipindi hiki cha kutafuta mtoto.

Inawezekana hii njia isifanye kazi mwezi wa kwanza tu wa huu mpango lakini ikafanya kazi mwezi unaofuata. Lakini kama mkeo ni mnene sana basi anza kwanza process za kushughulikia kupunguza unene wake. Maana hilo ni tatizo sana kwenye kushika mimba kuna tafiti kabisa zinazoonyesha kwamba asilimia kubwa ya wanawake wanene wana shida katika kushika mimba.

Nitashukuru kama utanipa feedback baada ya kufanikiwa.

Best wishes!
 
Kaka nashukuru kwa ushauri wako..kuhusu mke wangu wala si mnene anaumri wa miaka 29 na ana 62kg urefu 5ft. Unadhani vyakula hivi ntahitajika nitumie kwa kipindi gani? manake hali ya uchumi si nzuri sana
 
jaribu kwanza kwa hizo week mbili, tangu mkeo atakapoanza bleed na mkiwa mmesimamisha tendo la ndoa. kama itabaunsi basi itabidi ujitahidi uendelee na huo utaratibu kwa muda zaidi. Lakini kwa neema ya Mungu naamini ukizingatia vema ushauri wangu wa hapo juu, wiki mbili hizo za tangu kuanza bleed hadi siku ya kumi na tatu au kumi na nne zinatosha kabisa kufanya Mambo. Bwana Yesu na awe nanyi katika maombi yenu!
 
Kuweni na timing ya siku ya kufanya tendo husika,...Mimi nina group B negative na mume O positive na tuna watoto 2,Wakiume na wakike.USIWE NA WASIWASI
 
Mmejaribu kufanya follicular study (kuangalia lini mayai yanapevuka?). Sio.wanawake wote wanapevusha mayai siku ya 11 hadi 14. Tafuteni gynae mzoefu aangalie factors zote.
 
Uzuri wa sayans, iko very dynamic. Sasa hivi hata watu wanaotofautiana rhesus facor wanaweza kuzaliana vizuri tu kwa msaada wa daktari. Kuna sindano mama anachomwa wakati wa kujifungua. Lakini ni muhimu kuzaa mfululizo kwa sababu mwili wa mama unapoendelea kukaa unatengeneza antibodies dhidi ya hiyo combination.
Hizo rhesus factors ni blood protein ambazo ndizo zinazofanya hiyo blood group yako iitwe O positive au negative. Kwa hiyo wakisema ni positive ina maana kuna hizo protein zinazoitwa rhesus factor na ikiwa negative ina maana hizo rhesus factor hazimo. Kama itatokea mama akawa hana hizi protein halafu amepata mimba kutoka kwa mwanaume mwenye nazo, huwa zinatabia ya kufanya kitu kinaitwa blood clotting ambayo ni kama kuganda kwa damu ya mtoto na hivyo mimba iliyotungwa inaweza kuharibika tangu ikiwa tumboni au mtoto akafariki mara tu baada ya kuzaliwa.

Ila hiyo recessive gene nafikiri itakuwa kazi ngumu sana kukueleza, kwa maana inahusika na mambo ya crossbreeding kwenye mambo ya genetics. Sasa hilo litakuwa ni soma refu. Cha msingi elewa kwamba wewe na mchumba wako mna mbegu zinazofanana kwa hiyo mtapata mtoto
 
Kumbe kuna kundi jipya la blood group AO?
Msenyele kama wewe ni mwanabiolojia unajua kabisa kwamba crossing ya A na O italeta AO, lakini kwa kuwa O ni recessive, hiyo O haitaexist kwa hiyo itabaki kuwa A. Hapo nimeweka AO kwa ajili tu ya ufafanuzi kwa huyu mwenzetu.
 
Last edited by a moderator:
pole sana lakini hii swala la blood group sijiu kama linafanya kazi hata mimi ninatatizo hili mke wangu na mimi tuna A+ tumezaa mtoto lakini mpaka leo hii tuna mtoto mmoja tu na ana miaka 6 tukitaka ktafuta mwingine inakuwa issue sana mpaka leo hii nimeamua kumuachia Mungu maana yeye ndiye muweza
 
sisi wote ni O positive
mwanamke akiwa na grop yoyote ambayo ni -negative na mume akawa group yoyote +positive hapo ndo inakua ishu kupata mtoto[ japo si shida sana kupata mtoto wa kwanza] watoto watakaofuata ndo itakua ishu ngumu hadi achomwe sindano ya ant D vinginevyo atakua ashiki mimba, mimc zitatoka au watoto kufia tumboni.
 
Kubwa kabisa uwe na amani pia Muombe sana Mungu
 
Back
Top Bottom