Hawa watoto ndio maana wanafail aisee

Hawa watoto ndio maana wanafail aisee

AAAAh mkuu mi naomba namba yake tu ya simu tafadhali tena umesema mzuri duh. maisha yenyewe mafupi ila kumbuka yanaweza kuwa marefu pia.
 
Rafiki yako ana nia nzuri na wewe..kama vpi lete namba ya hako kabinti kazuri nikashughulikie.
 
Kweli we ni bunju . Embu nitupie namba yake na hutaona akikusumbua tena .
 
Juma anasema
Tia chai Roza
Tia maziwa
Tia Sukari...

Juma na Roza wanasoma shule
Shule yao inaitwa Mtakuja.
Ni Shule nzuri
Ina bustani za maua na matunda.
 
Kaka Sangarara asante sana kwa kushare experience na sisi. Nami naomba namba yake ili nikuepushie matatizo kwenye ndoa yako. mbona mimi ambae sijaoa havinisumbui sana zaidi ya salamu tu asbh nikienda kazini? au niko serious mno? usisahau kunipa nmba, kama yeye alivyopata namba yako, basi na mimi naomba namba yake
 
Usijaribu kuendelea na mazungumza na huyo binti na wala usimhusishe mama wawili kwani hakuna issue ya kujadli naye zaidi ya kujiongezea stress zisizo na msingi kwenye ndoa yako. Nenda kwenye simu yako na block hii namba kwa usalama wako vin
ginevyo umekwisha!
 
Sidhani kama hii issue ni kubwa kiasi hicho
Kwanza mlaumu sana huyo rafiki yako kwa kugawa namba yako bila ridhaa yako maana hiyo ni mbaya sana
Pili mweleze wazi huyo binti anayejua kuwa una mke na watoto bado anakufuata kutaka kuiharibu familia yako
Mwambie wazi kuwa huna mpango huo (kama kweli una nia ya kufanya hivyo maana unaweza kuwa na roho ya sitaki nataka) na unaiheshimu ndoa yako na suala sio kuwa una mke mkali wala nini ila unamuheshimu na unamheshimu mke wako
Na epuka mazingira ya kukutana nae au kukaa nae sehem ambako mko wawili tuu maana hiyo ni hatari nyingine (iwapo chanya na hasi zikikaribbiana)
 
Zingatia ushauri wa Rocky kijana!
 
wewe si una bakora? mchape kwa sanaaa...hata rudia tenaa!!! mchape kisawasawa!
 
Wengine huwa hayo matatizo hatuna kwani sura zetu zimekaa kijeshi jeshi. Binti akikuangalia tu mwenyewe anakuwa mpole na anaachana na wewe.
 
Kuna Binti mmoja kutokana na uzuri wake ililazimika abaki kwenye kumbu kumbu zangu
tangu mara ya kwanza tukutane Dukani Jirani na Maskani yangu. Baada ya nazani nilifanikiwa
kumuona mara ya pili akiwa amevaa school uniform ndo nikajua kwamba ni Mwanafunzi.

Sasa Jana Jioni, baada ya kufika home nikalazimika kwenda Bar Jirani na nyumbani ili nipate
serengeti zangu ndogo za baridi, nilipofika Bar nikakutana na Kijana mmoja mjanja mjanja
sana, na kafunga ndoa hivi karibuni, alikuwa akiingia Bar kama mimi, na sababu hatujaonana
muda mrefu tulipokariaba tukaanza kupeana salamu, hagi nyingi, vicheko, gonga sana mikono.
Haya yote tulifanya tukiwa jirani kabisa na meza ambayo kuna mabinti watatu walikuwa wamekaa
na sikuwa nimewali sababu niliishawapa mgongo pia by the time,

Sasa Jamaa akaniuliza, vipi wife kaishajifungua, sikumjibu bali nilimtolea simu na kuanza kumuonyesha
picha za uzao wangu, twe twins. a baby boy and a baby girl, nikamtajia na majina yao, sasa
huku jamaa akiwaanawashangaa matwins wangu kwenye simu, nikamsikia binti mmoja katika wale watatu
anayarudia majina ya watoto wangu, nikageuka kumuangalia, na yeye akawa ananiangalia, ikabidi nimpe
tano (nikagonga nae) huku namuambia uko juu hayo masikio sio ya kawaida - Na alikuwa ni yule
binti mzuri mwanafunzi. ndo apo nikagundua kumbe anapiga mvinyo pia, maswali mengi sana
yakapita kichwani mwangu muda huo huo, lakini nika let it go.

Then Jamaa huyu akaniambia vipi, karibu tukae mi niko na dada zangu hapa, nikakwepa, nikamueleza kuna
mtu namsubiri tunamaongezi hivyo ngoja nikakae palee, nikamplease kidogo na yeye akanielewa.

Cha Hajabu
Wakati naanza Serengeti ya Pili, Yule Jamaa akaja, akaniuliza, una mfahamu yule binti, nikamuuliza yupi,
akaniambia yule kanyoa nywele (binti mzuri), nikamueleza navyo mjua, na kwamba hata Jina wala anaishi
wapi au kusoma wapi sijui.

Jamaa Akafunguka
Hoo Binti anakaa na dada yake mtaa wetu huo huo (huyu kijana anaishi mbali ha hapa kidogo), akanielekeza
nyumba, na akaanza kunieleza anaishi na nani, ikabidi nimuwahi, kwani vipi? Hoo unajua huyu binti pale
kaja na rafiki zake, ili mimi kaniagiza kwako. "nikasema kimoyo moyo kazi imeanza". Oooh anakufahamu
sana, na amefurahi sana pale mlipogongesha mikono, "nikajua hili gemu kali". Oooh, na ameishaambiwa
mke wako mkorofi sana hivyo anaomba tuhame hapa twende sehemu ingine ana maongezi na wewe.
Nikamuuliza Jamaa, wewe unafanya nini na wale mabinti, mnaongea nao nini? Jamaa akaniambia tutaongea
mbele, akaniuliza tunaenda wapi. nikamuambia akamuuliza huyo binti anataka twende wapi, Ile Jamaa
anasimama tu kuelekea kwenye meza ya wale mabinti. Nikampigia simu wife aje Bar haraka sana, na fasta
nikawaagizia ile meza vinywaji na nikalipa. Wife alipikuja nikamuambia nikamuambia nilijisau kuja na pesa
Bar kwa hiyo kama kaja nayo anilipie bia mbili tuondoke, akakubali akalipa na tukaondoka. nikawa
nimemkwepa Ibilisi.

Tatizo ni kwamba, Nimeamua kutoa mchapo huu, sababu mchana huu, Nimepokea message iliyotoka kwa
huyo binti inasema
"Babbie, Pole na Kazi, Jana Mke wako aliharibu mipango yetu, mi nshatoka shule, naomba unieleze nikufuate
wapi ukishatoka Job, Loving you. Jina"

Hapa nimechanganyikiwa, namtafuta huyu rafiki yangu kwenye simu kumuuliza kwa nini kampe yule binti
number yangu, simu haipatikani. Na ninajiuliza huyu mtoto nikimkimbia zaidi na ndio kaanza kutuma mimessage
hili swala litajulikana kwa mama wawili sasa hivi.

Naomba ushauli wenu, ninachokifikiria nimuelekeze sehemu tukutane alafu nimcouncil kujihepusha na haya
mambo. Au ndio ntakuwa natenda wema kupita uwezo???

nipatie hiyo namba ya binti kwa PM
 
Kutana naye umwambie huhitaji hicho anachofikiria, na umwambie wazi huhitaji mawasilino naye. Ukicheza na mbwa ....
 
Salaaaaale !!!!!!!! Na mama wawili kesha stukia. Sijui nani kamtonya. Uswahilini kuna vituko.
 
Ninachokifikiria ni kwamba, baada ya meeting ya, kakiendelea kunisumbua naliwasilisha nyumbani mwenyewe
wife anisaidie
.

Mkuu yamaanisha hauna maamuzi yako binafsi hadi mkeo akusaidie????
Kuwa mwanaume mwenye maamuzi ya busara badala ya kujiharibia ndoa yako kisa kibinti km hicho.
Angalia usije mletea ngoma mama wawili, akashindwa kuja walea watoto wenu bureee. :A S-coffee:
 
Achana na vitoto vya shule vitakuletea matatizo.
 
Back
Top Bottom