MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Kiukweli ninashangazwa sana na tabia za hawa watu. Hawa wazee wa mambo ya bitcoin, cryptocurrency, betting na mengine yanayofanana na hayo wana shida gani kwenye vichwa vyao? Yaani vijana karibu wote wanaofanya hizi ishu kwa hapa Afrika lazima wawe na tabia za show offs na kujisifu mno huku wakijifanya washauri.
Je, unapoingia kwenye hizo kazi huwa kuna mafunzo ya siri ya namna ya kujisifu? Sina tatizo na wao kupiga hela ila haiwezekani wakapiga hela bila makelele kama watu wa kwenye shughuli zingine? Wapo vijana kibao kwenye kilimo, michezo, sanaa, na kazi zingine nyingi wanapiga noti ndefu sana ila huwezi kusikia makelele kama ya hawa vijana wa forex na betting.
Nini chanzo cha haya? Tatizo limeanzia wapi? Wanapata manufaa gani kwa kujisifu kuwa wana pesa?