Hawajamaliza: Mabando ya data kupanda tena upya, Naibu spika ampa kibarua Nnape kupandisha gharama

Hawajamaliza: Mabando ya data kupanda tena upya, Naibu spika ampa kibarua Nnape kupandisha gharama

Fungua kinywa chako tujue kiwango cha busara au upuuzi wako,
Huyu tunamuweka wapi kwa mapendekezo yake hayo?
 
Bado hawajamaliza,

Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Mussa Azzan Zungu, amemtaka Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe.Nape Nnauye, kuona namna watakavyoweza kushirikiana na Wizara ya Fedha, kuja na mfumo thabiti utakachochea ongezeko la mapato ya serikali kupitia matumizi ya data.
Hawa wanawaibia wananchi wa255 iko hivi.. kipindi cha utawala wa Jk alitumia akili nyingi kama tunavyojua Tz haijawahi pata raisi mjanja kwenye mambo ya Teknolojia kama Jk..
Jk alijenga mkonga wa mawasiliano uliopita baharini mpaka hapa kwetub Tz.. hii program ilifanyika miaka ya kuanzia 2011 hivi kama sikosei ikatufanya Tanzania tuwe na gharama nafuu za huduma ya mawasiliano tofauti na nchi zilizotuzunguka..

Kwa kuwa na gharama ndogo ilipelekea nchi jirani kuomba kuunganishwa pia.. nchi hizo ni Zambia,Malawi,Rwanda,Uganga na Kenya.

Miaka ikaenda gharama zikiwa nafuu Tanzania mpaka Jk alipomaliza madaraka akamkabidhi kijiti Hayati JPM.. hapa zikaanza kupanda ila sio kiihivyo sasa baada ya utawala kuja wa wajanja huu [emoji23] [emoji23]. Kwa akili zao wanajua watanzania ni wasahaulifu na sio wafatiliaji wa mambo gharama wanapandisha maradufu kumkomoa mtanzania bila kujali cake inaliwa na wachache hii kupitia Data.. kuwa kumbusha tu huo mkonga wa mawasiliano ndio uliopeleka Internet mlima Kilimanjaro mwezi uliopita

Na ukizingatia sahivi Internet ni hitaji muhimu kutokana na dunia tunayoishi kwa sasa.. wanafunzi wanapata tabu kujifunza maarifa muhimu kwaajili ya gharama kuwa juu na bado hawaoni kama wanaharibu next generation kushindwa kupambana na soko la dunia kwenye ajira n.k
 
Nchi inaongozwa na Mapaka👇😁😁😁
AEb8rs.jpeg
16525976734300.jpg
ummY_jc.jpg
AEb8rsjc.jpeg
 
Huyu ni zaidi ya mtumbwi wa kibwengo. Wananchi tujilaumu wenyewe Hivi unamchaguaje mtu wa aina hii awe mwakilishi wako bungeni?
Wapo wamejaa bungeni wanatafuna kodi zetu tu. 2025 watu wa aina tusiwape tena nafasi.
Aliwasimika jiwe. Hakuna mwananchi anaweza kumchagua huyo jambazi muuza ngada
 
Bado hawajamaliza,

Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Mussa Azzan Zungu, amemtaka Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe.Nape Nnauye, kuona namna watakavyoweza kushirikiana na Wizara ya Fedha, kuja na mfumo thabiti utakachochea ongezeko la mapato ya serikali kupitia matumizi ya data.
Bure kabisa hii sirikali
 
Huyu ni zaidi ya mtumbwi wa kibwengo. Wananchi tujilaumu wenyewe Hivi unamchaguaje mtu wa aina hii awe mwakilishi wako bungeni?
Wapo wamejaa bungeni wanatafuna kodi zetu tu. 2025 watu wa aina tusiwape tena nafasi.
Usipowapa kura, watapita tu .
Problem ni mfumo.
Katiba mpya ndio mtetezi wa wanyonge.
Hao ni familia moja, hawana shida na mtu.
 
Kuchochea ongezeko la mapato inatakiwa kupunguza kodi na tozo ili wananchi wengi washiriki katika kufanya matumizi na kuchangia pato la taifa.
1.Punguza kodi ya uagizaji wa magari,wamiliki wawe wengi,mafuta yanunuliwe kwa wingi na kodi iongezeke.
2.Miji,viwanja,makazi na mashamba yapimwe kwa 'satellite's ili kurahisisha mipango miji na kuweka mazingira rahisi ya uwekezaji.
3.Msamaha wa kodi utolewe kwa wawekezaji watakao wekeza mikoa ya pembezoni,na hii itachochea kufungua ajira na bidhaa itakayozalishwa itatozwa kodi na hivyo kuongeza mapato.
4.Punguza kodi kwa watumishi(P.A.Y.E),au Serikali iongeze mshahara ili kuchochea matumizi(rejea mfano namba 1 hapo juu).
5.Ruhusu baa kuwa na leseni za "night club" ili kuwe na muda mrefu wa wananchi kufanya matumizi na hivyo kuchangia mapato.
6.Kwa nini kama nchi tuna lala mapema? Usafiri na shughuli za kiuchumi ziendelee hadi usiku na mzunguko wa fedha utaende saa 24,pato la taifa litaongezeka.(Zuio la kusafiri usiku liangaliwe na kufanyiwa tathimini).
7.Shughuli za kiuchumi na kijamii zikiendelea kwa saa 24,ajira zitaongezeka🙁wapo watakaofanya kazi usiku na wapo na mchana).
8.Bunge lijikite katika kurekebisha sheria ambazo ni kikwazo katika kuchochea ukuaji wa pato na mzunguko wa pesa katika taifa(Bunge liangalie na kupitia sheria zinazochelewesha taifa kuelekea uchumi wa kati (rejea mfano namba 1,5 na 6 hapo juu).
 
Bado hawajamaliza,

Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Mussa Azzan Zungu, amemtaka Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe.Nape Nnauye, kuona namna watakavyoweza kushirikiana na Wizara ya Fedha, kuja na mfumo thabiti utakachochea ongezeko la mapato ya serikali kupitia matumizi ya data.
Wazo la Zungu ni zuri ila Waziri asilitekeleze maana litakuwa ni zigo lake..

Tozo za miamala zimeonesha ni zigo la Mwigulu na sio Rais Wala Serikali..
 
Back
Top Bottom