Vitu vingine ni aibu hata kuvisoma, unasomaaaaaà mwisho wa maoni unajaribu kupima aliyeandika haya ana hali gani kiafya (afya ya fahamu) unabaki kumhirumia tu labda ana msongo wa mawazo, au upeo wake siyo wa kujadili jambo hili au anatumikia Kafiri ili apate mradi wake!!?
Mtu anaona sheria yoyote mbovu inayopitishwa Bungeni tena kwa malengo binafsi ya kakikundi ka watu haimhusu, anadhani sheria kandamizi ni kwa ajili ya kina Lema na Mdee. Hata Kinana hakutegemea kwamba kuna siku atalazimika kuomba radhi huku akiwa kakoksewa yeye. Nape hakutegemea kuna siku atatembelea magoti mita 120 kwenda kusujudu mbele ya binadamu mwenzake ili apewe ruhusa ya kufunguliwa geti akaombe msamaha pasipo na kosa.