Kiongozi hapo kwenye bold, inaonekana kinachomrudisha huyo jamaa si mapenzi ya kweli kwa mtalaka wake bali hiyo njaa yake na hiko cheo kipya cha ujaji alichokipata huyo mpenziwe wa zamani.
Kwa kutumia akili ya kawaida kabisa, inaonekana hata kama wakirudiana
inawezekana kabisa wakatengana tena maana sababu za msingi zilizofanya wapigane vibuti hazijatatuliwa na pia kinachowaunganisha kwa sasa
si upendo ila ni cheo cha ujaji na umaskini wa huyo mpiga kibuti na njaa zake!
Ingekuwa ni busara huyo mpiga kibuti asishadadie cheo cha mtalaka wake na kuendeshwa na njaa zake bali atumie nafasi yake ya kufanya kazi kwa bidii na ajipatie kipato kwa jasho lake mwenyewe badala ya kugeuka mwanaume kama binti ili kulinda hadhi na heshima yake kama mwanaume rijali na pia kusimamia misimamo na maamuzi yake binafsi!
HorsePower wakati mwingine njaa inakupa nidhamu hata kama ni ya uwoga.........kidume nionavyo safari akishikwa atashikamana maana khali yake haitii matumaini hata chembe