Hawara aua mama na wanae

Hawara aua mama na wanae

Mtanzania2020

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2020
Posts
817
Reaction score
1,752
Eva Stephano na watoto wake wawili wakazi wa mtaa wa Lwanima Ihushi wilayani Nyamagana, Jijini Mwanza wamefariki dunia kwa kuungua moto usiku wa kuamkia Desemba 7, 2023, baada ya nyumba waliyokuwa wakiishi kuchomwa moto na aliyedaiwa kuwa hawara wa mama huyo.

Akitoa taarifa hiyo Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza Wilbroad Mutafungwa, amesema walipokea taarifa ya nyumba hiyo kuwaka moto ndipo walifika na kufanikiwa kuwaokoa watu watatu waliokuwa wamelala ndani ya nyumba hiyo huku mama mwenye nyumba hiyo aitwaye Eva Stephano na watoto wake wawili wakifariki dunia kwa kuungua moto.

Aidha Kamanda Mutafungwa amesema baada ya kuchunguza tukio hilo ilibainika lilihusishwa na wivu wa mapenzi ambapo aliyehusika kuchoma moto nyumba hiyo alikuwa hawara wa mwanamke huyo na Jeshi hilo linaendelea na msako mkali ili kumkamata na kumchukulia hatua za kisheria.

#EastAfricaRadio

FB_IMG_1702049994040.jpg
 
Matatizo mengi ktk mahusiano yanatokana na wawili wapendanao au wanao-ektiana kupendana kukosa uaminifu.

Bahati mbaya sana hao ndiyo wengi wamejaa dunia hii.
 
Back
Top Bottom