May Day
JF-Expert Member
- May 18, 2018
- 6,311
- 9,027
Mara nyingi wanapotajwa Manguli wa Muziki wa Rege Duniani sidhani kama hata jina la Eric Donaldson litakumbukwa....Mara nyingi atatajwa Bob Marley, Peter Tosh, Burning Spears, UB 40 n.k.
Nguli huyu mwenye miaka 73 sasa ni moja ya Watu waliojaliwa sauti nzuri isiyozeeka, inayovutia kwenye masikio ya msikilizaji yeyote.
Kibao kama Cherry oh baby sidhani kama wengi wetu watakwambia Mtunzi wa awali ni Eric na sio UB 40 kama wao walivyopata umaarufu kupitia kibao hicho...si mwenye makeke sana nadhani ndio sababu haswa ya kuchukuliwa wa kawaida na mashabiki wengi wa Muziki wa rege.