Hawavumi lakini wapo. Eric Donaldson nguli wa rege wa Jamaica

Hawavumi lakini wapo. Eric Donaldson nguli wa rege wa Jamaica

May Day

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2018
Posts
6,311
Reaction score
9,027
Eric 20.png

Mara nyingi wanapotajwa Manguli wa Muziki wa Rege Duniani sidhani kama hata jina la Eric Donaldson litakumbukwa....Mara nyingi atatajwa Bob Marley, Peter Tosh, Burning Spears, UB 40 n.k.

Nguli huyu mwenye miaka 73 sasa ni moja ya Watu waliojaliwa sauti nzuri isiyozeeka, inayovutia kwenye masikio ya msikilizaji yeyote.

Kibao kama Cherry oh baby sidhani kama wengi wetu watakwambia Mtunzi wa awali ni Eric na sio UB 40 kama wao walivyopata umaarufu kupitia kibao hicho...si mwenye makeke sana nadhani ndio sababu haswa ya kuchukuliwa wa kawaida na mashabiki wengi wa Muziki wa rege.

Aaah kumbe, hiki kibao kinanikumbusha enzi za utoto wangu nikiwa na bro wangu kwenye landrover 110 ameweka tape imejaa ngoma za raggae ambazo mpaka leo natamani zipata lakn sijui aliimba nani na zinaitwaje. Ila ni ngoma ambayo naipenda sana.
 
Jamaa ana uwezo mkubwa ingawa hatajwi sana.
 
Umenikumbusha trafic light.....

take a ride in a mini bus
Destination kingston, kingston
Sudden we come to a stop
Then i look around.....

Old good days
 
Umenikumbusha trafic light.....

take a ride in a mini bus
Destination kingston, kingston
Sudden we come to a stop
Then i look around.....

Old good days
Kuna ile ya "cherry oh cherry oh baby"...UB 40 waliirudia wakapata nayo umaarufu sana.
 
Umenikumbusha mbali sana jamaa, haswa kitu cha papaa pipi.
 
Pipiii ,red light. jamaa anakisauti fulani cha ajabu hivi visauti hata Ritchie Spice nae anacho.
 
Pipiii ,red light. jamaa anakisauti fulani cha ajabu hivi visauti hata Ritchie Spice nae anacho.
Ndio maana nikaweka na picha yake, Watu wakiona Muimbaji wengi watakuwa suprised.
 
Back
Top Bottom