Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 23,526
- 34,057
Wewe mzee utaachaga lini utapeli?
PUBLICATIONS/RESEARCH PAPERS/ARTICLESWewe mzee utaachaga lini utapeli?
ni kama tu shehe mwaipopo wote wako kwenye payroll ya islamists ...
Ni bora ukose hela ila sio kukosa akili. Kila ukiamka unaamka na maneno ya kudhihirisha na kuonyesha wazi namna ulivyopunyuka hekima na maarifa ya kimaisha.
Sasa waislamu chuo chao kina elimu gani ya maajabu ambayo inawatofautisha na raia au vyuo vingine na kuwapa access ya kupata ajira kama raia wengine?
Unajua wewe ni huna akili ile ya kukosa akili na kuwa mjinga kabisa?🤔
Wewe ni mdini wa wazi kabisa na haya mambo sisi watanganyika hatuyataki kuhibiriwa hekaya na watu washenzi na wafitini kama wewe ambao lengo lao ni kuleta mifarakano ndani ya jamii ya watanganyika.
Wewe kama unahusudu sana hiyo dini yako nenda pale uhamiaji omba passport 🛂 uende Saudi Arabia au taifa lingine lolote ambalo ni la kiislamu ukaishi huko. Hizi akili za kis*ng* za kupenda kuanzisha mijadala ya kujionyesha kuwa waislam ni victim na wanaonewa na raia wenzao wakati TANGANYIKA hakuna mifumo ya kubagua raia na huwezi kuta mifumo ina halalisha raia awe anabaguliwa kwa dini.
Nenda mataifa yanayoishi kiislamu kama huko Saudi Arabia,Iraq, Iran kaishi huko hautapata mazingira ya kuchangamana na watu wa dini tofauti na wewe.
Hatuwezi kuwa tunasikiliza malalamiko ya kibaguzi na ya kipuuzi kama haya na kuacha kudili na malalamiko ya kimaendeleo yanayomlenga kila mtanzania at large.
Punguza ufala.
Huko saudi hawezi Kwenda atakimbilia uingereza kwa makafiriNi bora ukose hela ila sio kukosa akili. Kila ukiamka unaamka na maneno ya kudhihirisha na kuonyesha wazi namna ulivyopunyuka hekima na maarifa ya kimaisha.
Sasa waislamu chuo chao kina elimu gani ya maajabu ambayo inawatofautisha na raia au vyuo vingine na kuwapa access ya kupata ajira kama raia wengine?
Unajua wewe ni huna akili ile ya kukosa akili na kuwa mjinga kabisa?🤔
Wewe ni mdini wa wazi kabisa na haya mambo sisi watanganyika hatuyataki kuhibiriwa hekaya na watu washenzi na wafitini kama wewe ambao lengo lao ni kuleta mifarakano ndani ya jamii ya watanganyika.
Wewe kama unahusudu sana hiyo dini yako nenda pale uhamiaji omba passport 🛂 uende Saudi Arabia au taifa lingine lolote ambalo ni la kiislamu ukaishi huko. Hizi akili za kis*ng* za kupenda kuanzisha mijadala ya kujionyesha kuwa waislam ni victim na wanaonewa na raia wenzao wakati TANGANYIKA hakuna mifumo ya kubagua raia na huwezi kuta mifumo ina halalisha raia awe anabaguliwa kwa dini.
Nenda mataifa yanayoishi kiislamu kama huko Saudi Arabia,Iraq, Iran kaishi huko hautapata mazingira ya kuchangamana na watu wa dini tofauti na wewe.
Hatuwezi kuwa tunasikiliza malalamiko ya kibaguzi na ya kipuuzi kama haya na kuacha kudili na malalamiko ya kimaendeleo yanayomlenga kila mtanzania at large.
Punguza ufala.
Huko saudi hawezi Kwenda atakimbilia uingereza kwa makafiri
Huyu mzee ni mjinga mjinga sana
Economist,Nyerere alituokoa sana na Hawa wafia dini.
Usitake kutuchanganyia habari. Hakuna mtu alimpa kitu mtu. Nyerere ni mwanasiasa kama wengine na alitumia influence yake kisiasa katika uasisi wa kulijenga hili taifa.Economist,
Ili uweze kuchangia mada hii kwa uhakika unahitaji uijue historia ya Mwalimu Nyerere katika siasa.
Mwalimu Nyerere amefika Dar es Salaam mwaka wa 1952 na akapelekwa kwa Abdulwahid Sykes Act. President na Secretary wa TAA na Joseph Kasella Bantu.
Hapa ndipo unapotakiwa uanzie.
Nyerere kaikuta TAA inaongozwa na TAA Political Subcommittee iliyokuwa na wajumbe hawa: Mufti Sheikh Hassan bin Ameir, Said Chaurembo, Hamza Mwapachu, Abdulwahid Sykes, Steven Abdallah Mhando, John Rupia na Dr. Vedasto Kyaruzi.
Unathitaji halikadhalika uwajue waasisi wa TAA (African Association) nakuwekea majina yao: Kleist Abdallah Sykes, Mzee bin Sudi, Ibrahim Hamisi, Suleiman Majisu, Zibe Kidasi, Ali Said Mpima, Raikes Kusi, Cecil Matola na Rawson Watts.
Video hiyo hapo chini itakamilisha historia ya Mwalimu Nyerere:
View: https://youtu.be/oLkefadOoJ0?si=5kkeHcsnZBnviK84
Ingekuwa wazee wangu wabaguzi wa dini Hamza Mwapachu na Abdulwahid Sykes wasingekubaliana kumpa Nyerere uongozi wa TAA mwaka wa 1953 katika uchaguzi uliofanyika Ukumbi wa Arnautoglo tarehe 17 April wapiga kura wengi wao wakiwa Waislamu.
Zemanda,Usitake kutuchanganyia habari. Hakuna mtu alimpa kitu mtu. Nyerere ni mwanasiasa kama wengine na alitumia influence yake kisiasa katika uasisi wa kulijenga hili taifa.
Ukisema hao wazee wa kislamu ndio chanzo cha uhuru wa taifa na walimpa Nyerere mamlaka na bila wao isingewezekana then ni wazi wewe unapotosha kwa kuongea kipande kidogo cha eneo kubwa.
Kuna wachagga,walikuwa na mfumo wao wa machifu ila waliachana nao na kusikilizana na mwalimu nyerere ilipokuja swala la uhuru,je na wao waseme wana umuhimu kushinda wengine?
Kuna watemi wa makabila mbali mbali kama wahehe, wajita,wakurya, wamasai,wasukuma.
Hawa ni watanganyika waliokuwa na mifumo yao ya kitawala la machifu ila walikuwa wapole mbele ya mwalimu na hawakuendelea na mifumo yao wakakubali kuwa sehemu ya jamuhuri ya watu wa TANGANYIKA.
Wewe leo unakuja na hekaya za elfu lela ulela na kututungia uongo wa kutengeneza hapa. Aliyekwambia kuwa uhuru lilikuwa ni ajenda ya waislamu ni nani kwanza kwamba TANGANYIKA nzima ni waislam kwamba hakuna watu wengine walishiriki issue ya kutafuta uhuru,yaani umeamua kuwa selective kwa kutazama majina ya dini tu? Vingine huoni?
Sikiliza wewe mzee uliyemaliza muda wako wa ujana na sasa upo uzee, huu sio wakati wa kuanza kutenganisha vijana na kuwapa fikra za ubaguzi wa kidini,sio kizazi hiki. Hizo fikra zako ishi nazo mwenyewe sisi kama vijana hatuzihitaji na tunaishi kwa mifumo ya sasa.
Sawa unaelezea matukio ya kihistoria ila unapofeli ni kubagua kwa misingi ya kidini kwa kudogosha nguvu na jitihada za washiriki kwa kuwatambua zaidi waliokuwa na majina ya kiarabu na kuwaweka kando waliokuwa na majina yasiyo ya kiarabu.Zemanda,
Tuanze mwaka wa 1924 Dr. Kweggyr Aggrey alipokuja Tanganyika na akakutana na Kleist Sykes.
Dr. Aggrey ndiye aliyempa Kleist Sykes wazo la kuunda African Association.
Waasisi wa African Association ni hawa: Cecil Matola (President), Kleist Sykes (Secretary), Mzee bin Sudi, Ibrahim Hamisi, Suleiman Majisu, Ali Said Mpima, Zibe Kidasi, Rawson Watts na Raikes Kusi.
Huu ni mwaka wa 1929.
Majina haya yamefutwa hayapo popote katika historia ya uhuru wa Tanganyika.
Historia hii haipo.
Nani anaepotosha historia hii?
Mimi ninaeeleza historia hii au walioifuta?
Tumewataja Wachagga na Mangi wao.
Chief Abdul Shangali wa Machame TANU inaingia Moshi Mjini yeye Member wa Legislative Council.
Thomas Marealle yeye Paramount Chief wa Wachagga anaongoza Chagga Council.
Thomas Marealle na Abdulwahid Sykes walikuwa marafiki wakubwa.
Nimesoma barua za Chief Thomas Marealle alizokuwa anamwandikia Ally Sykes wakati wa kupigania uhuru.
Mambo mazito.
Mangi hawakuiunga mkono TANU.
TANU iliasisiwa na Yusuf Olotu akishirikiana wazalendo kama Juma Ngoma, Mama bint Maalim, Halima Selengia, Amina Kinabo, Lucy Lameck na wengineo.
Muasisi wa TANU Joseph Kimalando hakutaka kusajili chama.
Ally Sykes ndiye aliyempa maagizo Yusuf Olotu wasajili TANU bila Joseph Kimalando.
Tumewataja Wahehe.
TANU ilipelekwa Iringa na Abdul Sykes na Dossa Aziz na kadi ya kwanza Iringa ni ya Chief Adam Sapi Mkwawa.
Aliyeieneza TANU Iringa ni Abbas Max na Abbas Max aliingizwa TANU na Abdulwahid Sykes.
Umeghadhibika.
Unaniita, "Wee Mzee."
Hii ni dharau.
Hakika mimi ni kikongwe miaka 74 SI kijana tena.
Lakini ndiyo unitukane kwa kukueleza historia ya kweli ya TANU?
Haya yote ni kweli tupu na si hekaya wala Alfu Lela Ulela.
Hayo mengine sijaona umuhimu wa kuyasemea.
Zemanda,Sawa unaelezea matukio ya kihistoria ila unapofeli ni kubagua kwa misingi ya kidini kwa kudogosha nguvu na jitihada za washiriki kwa kuwatambua zaidi waliokuwa na majina ya kiarabu na kuwaweka kando waliokuwa na majina yasiyo ya kiarabu.
Mzee umri sio hekima. Unaweza kuishi miaka mingi ila haukuwa umejifunza mengi kama wazee wenzako.
Hizi fora unazozijenga hapa ni wazi kuwa wewe si mtetezi wa ukweli bali mpandikizi wa chuki na udini kwa vijana wadogo ndio maana umekazana sana kuonyesha kuwa kuna watu walionewa au kufunikwa katika historia.
Haiingii akilini kuwa movement yote ya kipindi cha harakati za uhuru iwe dominated na waislam kwa 100% huu ni upotoshaji wa historia na lengo ikiwa ni kupandikiza mbegu ya chuki katika jamii ya sasa.
Na nadhani hii mnafanya kusudi ili kwa msukumo kutoka Zanzibar. Wazanzibari wanaoishi bara mnahofu sana na muungano ukivunjika watakosa mtetezi ndio maana wanajishikamanisha sana na udini ili kuwakoroga watanganyika watofautiane na kugawanyika kwa misingi ya udini.
Wazanzibari eneo lao ni square kilometers 4,000 haliwezi kuongezeka labda wajaze kifusi baharini. Kwahiyo namna rahisi ya kujipanga ni kuanza kufosi expansion huku TANGANYIKA kwa kutengeneza udugu feki na waislam wa TANGANYIKA na kuanza kutengeneza migogoro na watanganyika wengine ili waikorofishana ninyi muwe na advantage ya kupata watu wa kuwasitiri na kuunda nao udugu ili mpate ardhi ambayo sasa hamna. Shughuli za wazanzibari za kiuchumi kwa sasa 90% wapo ardhi ya TANGANYIKA.
Hilo tumelijua na tumeshawashitukia. Mnataka ardhi ya TANGANYIKA kama vile Rwanda wanavyotaka ardhi ya Kongo, kwa kutengeneza migogoro ili kusitawalike wao wachukue eneo kubwa kwasababu idadi ya watu wao inaongezeka eneo haliongezeki.
Sisi sio wajinga mzee. Miaka yako 74 unakazana na udini unataka kutuchorea historia kwa kutumia hisia zako?
Tukianza kuwachimba hao unaotaja hapo naweza kukujia na taarifa kubwa kushinda hao unaowataja kwa kutengeneza. Wewe unataja mtu m'moja na unampamba kwa udini mimi ntakuja na watu hamsini na sitawapamba kwa udini.
ACHA UPOTOSHAJI MZEE,HIZI CHUKI UNAPANDIKIZIA ZA UDINI WAJUKUU HAWATAKUWA SALAMA NA MWISHO WA SIKU HAUTAKUWEPO KUWAONA WAKIPIGANA HIZO NGUMO UNAZOTAKA WAPIGANE.
Changamoto ni lugha yako mzee sio kwamba tunashindwa kuelewa unachosema ila msisitizo wako una msukumo wa udini.Zemanda,
Nami nakuulizia swali.
Ulitaka nisiwataje waasisi wa African Association?
Waliobagua ni wale waandishi wa historia hii waliowafuta Waislamu.
Laiti wangelitajwa mimi nisingeandika historia yao.
Unasema sijajifunza mengi kama wazee wenzangu.
Naomba unitajie hao wazee wenzangu unaowalinganisha na mimi.
Unajua nimeandika vitabu vingapi, nimealikwa vyuo vikuu vingapi kuzungumza?
Ningekuwa nina chuki nisingeombwa kufanya mahojiano na TBC, Daily News, Habari Leo wala nisingetiwa katika mradi wa Rais Magufuli wa kuandika upya historia ya Tanzania.
Hakuna popote niliposema Waislamu walihodhi harakati zote za uhuru kwa asili mia moja.
Kuhusu Zanzibar fungua uzi mpya tujadili.
Nimealikwa Zanzibar mara tatu kufanya pitio la vitabu kuhusu historia ya mapinduzi.
Nilikuwa Mtafiti Msaidizi wa Dr. Harith Ghassany kwa miaka minane wakati anatafiti kitabu chake "Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru."
Hayo mengine sikuyagusa kwa kuwa hayana maana.
View: https://youtu.be/bn9RRKMN9qA?si=7W-Y0c2kiGPkrqvm